****************
20,Juni
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MBUNGE wa jimbo la Mji wa Kibaha,mkoani Pwani Silvestry Koka amechangia malumali zenye thamani ya sh.milioni mbili kwa jeshi la polisi mkoani hapo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kujenga makazi ya askari polisi.
Akikabidhi malumalu hizo kwa kamanda wa polisi mkoni humo ,Wankyo Nyigesa ,Mbunge Koka alipongeza serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa makazi hayo ya askari.
Alisema askari wanafanya kubwa lakini makazi yao ni duni na mradi huo una manufaa na ni ukombozi kwao.
Koka alieleza ameamua kulisaidia jeshi hilo ili kukamilisha ujenzi huo ambapo Rais Dk John Magufuli alilipatia jeshi hilo mkoa kasi cha shilingi milioni 500.
“Tujitoleeni katika miradi kama hii,kutoa ni moyo ili kushirikiana na serikali kutimiza malengo yake na kufikia uchumi wa kati”alifafanua .
Nae Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa alimshukuru Mbunge huyo.
Alisema askari wengi hawana nyumba za kuishi hivyo kulazimika kuishi uraiani ambapo inakuwa ngumu kuwapata pale inapotokea dharura ya kikazi.