MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati akifungua semina ya wenyeviti wa Mitaa na Madiwani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Tanga a |
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim akizungumza wakati wa semina hiyo |
Mwakilishi wa Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Lucas Kaigarura ambaye ni Meneja Msaidizi Upande wa Madeni TRA Tanga |
Meneja Msaidizi Idara ya Forodha Edward Ndupa akizungumza katika semina hiyo |
Ofisa wa Elimu kwa Mlipakodi Mkoa wa Tanga Salim Bakari akizungumza wakati wa semina hiyo |
MKUU wa Kitengo cha Kodi za Majengo TRA Mkoa wa Tanga John Minja akieleza umuhimu wa ulipwaji wa kodi hizo wakati wa semina hiyo |
NAIBU Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu akizungumzaa |
Mwenyeviti wa Serikali Mitaa kwenye Jiji la Tanga Maimuna Ramadhani
kutoka Mtaa wa Mabawa Mikanjuni A akiuliza swali wakati wa semina hiyo
Diwani wa Kata ya Majengo (CUF)
Diwani wa Kata ya Msambweni Jijini Tanga (CUF) Abdurahamani Hassani katikati akiwa na madiwani wengine kwenye semina hiyo
Sehemu ya Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wakifuatilia semina hiyo
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka wenyeviti wa mitaa na
madiwani kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kupiga vita biashara za
magendo ikiwemo kuwafichua wanaohusika kwenye maeneo yao kwani vinawatia
doa.
Mwilapwa aliyasema hayo leo wakati akizungumza na madiwani na wenyeviti
wa serikali za mitaa katika semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa
na Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Tanga.
Alisema kwamba wilaya ya Tanga kuna tatizo kubwa hata wakati fulani Rais
Dkt John Magufuli alikwisha kutaja kwani miongoni mwa wilaya zenye
vipenyo vingi vya uingizaji bidhaa bila kufuata utaratibu kupitia
Bandari rasmi.
Mkuu huyo wa wilaya ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella kwenye semina hiyo alisema kwamba hivi sasa wamejipanga imara
kuweza kuhakikisha mianya yote haipitisha bidhaa kwa njia zisizo rasmi
kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali.
Aidha pia aliwataka viongozi hao kushirikiana na watu mbalimbali ikiwemo
kuhakikisha biashara na shughuli zinazoendeshwa ndani ya wilaya
zinakwenda kwa utaratibu unaokubalika.
“Lakini suala la biashara ya magendo tumekuwa tukiipigia kelele kila
wakati tumekuwa na tabia ya kuingiza bidhaa kwa njia za panya tabia hii
inatukera tumekuwa tukipambana nalo na tunaamini litakwisha
kabisa”Alisema
Mkuu huyo wa wilaya alisema anaamini semina hiyo itawapa uelewa mkubwa
ambao utakuwa chachu kwenye maeneo yao kwa sababu ni wanasiasa wana
ushawishi kwa jamii watumie njia mbalimbali kuweza kuwapa elimu jamii
itasaidia kupunguza na hatimaye kumaliza magendo.
“Lakini pia wataalamu na wanasiasa tukishikamana kwa pamoja tunaweza
kumaliza tatizo la magendo huku akiwataka viongozi wenye tabia za namna
hiyo kuachana nazo kwani wakikamatwa wataishi kwenye mikono ya
kisheria”Alisema
Awali akizungumza katika semina hiyo Mwakilishi wa Meneja wa TRA Mkoa wa
Tanga Lucas Kaigarura ambaye ni Meneja Msaidizi Upande wa Madeni TRA
Tanga alisema wameitisha kikao hicho cha madiwani na wenyeviti ili
kuwaelimisha masuala mbalimbali kuhusu kodi kwani wao ni nguzo kuu ya
wananchi ili waweze kuipeleka elimu hiyo.
Alisema pia semina hiyo imelenga kwenye umuhimu wa kodi,Masuala ya EFD
Mashine ,kutoa na kudai risiti,Elimu ya umuhimu wa kulipa kodi
mbalimbali ikiwemo ada za mabango kwa sababu wapo karibu na wananchi
wakifikisha huko inaweza kuwa chachu ya kuongeza mapato.
Hata hivyo alisema suala la magendo sio mazuri kwa sababu yanaikoseka mapato serikali hivyo wanaimani watafanikiwa kuliondosha.
Naye kwa upande wake Diwani wa Kata ya Msambweni (CUF) Abdurhamani
Hassani alisema baada ya elimu hiyo wamejifunza mambo mengi hasa suala
la magendo jambo ambalo linaathiri ukusanyaji wa mapato.
Alisema yapo magendo yanafanyika kutokana na kuwepo kwa uelewa mdogo kwa
wale wafanyabiashara kwa sababu ukitazama viwango cha kodi vinalipika
watajiahidi kwenye kueilimisha jamii kwa sababu kodi sio jambo la hiari
bali ni lazima.