Na.Alex Sonna,Dodoma
Jumla ya watu 168 wamenusurika na ajali ya Treni iliyotokea mkoani Dodoma katika maeneo ya level cross ya hazina katika halamshauri ya jiji la Dodoma.
Ajali hiyo imehusisha Gari lenye no za usajili T 860 APW aina ya isuzu likiendeshwa na Dereva Hamis Salamu (49) mkazi wa Nkuhungu ambapo gari hilo liligonga Treni ya abiria No, Y 12,ikiendeshwa na Michael Mdachi (44) mkazi wa kisasa Jijini hapa na Guard Abdala Ngola (59) ambaye ni mkazi wa Area c Dodoma.
Akizungumza katika eneo la tukio, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema Treni hiyo ilikuwa ikitokea kigoma ,mwanza na mpanda kuelekea Dar es salaam ikiwa na behewa 9 za daraja tatu mbili za daraja kwanza,Behewa la mgahawa moja,Behea la vifurushi moja na Behea la Breki Moja na kusababisha majeruhi kwa abiria 32 waliokuwa kwenye Behewa namba 3648 na 3607 ambayo yalianguka.
”Mnamo tarehe 17a ya 11/06/2019 majira ya saa 11:25 usiku ilianza safari kutoka Tabora kuelekea Dar es Salaam ikiwa na mabehewa 14 kama yalivyotajwa hapo juu na ilipofika maeneo ya kuvuka makutano ya Reli na kugongwa na gari”amesema Muroto
Muroto amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari alipokuwa akivuka makutano ya Reli na barabara hivyo gari kuzima likiwa katikati ya Reli na Dereva wa gari aliruka na kukimbilia Polisi Kujisalimisha
Aidha, kamanda muroto ameongeza kuwa hali ya abiria waliopata ajali hiyo kati ya abiria 32 watatu hali sio za kuridhisha.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobasi katambi ameliomba jeshi la polisi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kujua chanzo cha ajali hiyo.
Na.Alex Sonna,DodomaJumla ya watu 168 wamenusurika na ajali ya Treni iliyotokea mkoani Dodoma katika maeneo ya level cross ya hazina katika halamshauri ya jiji la Dodoma.Ajali hiyo imehusisha Gari lenye no za usajili T 860 APW aina ya isuzu likiendeshwa na Dereva Hamis Salamu (49) mkazi wa Nkuhungu ambapo gari hilo liligonga Treni ya abiria No, Y 12,ikiendeshwa na Michael Mdachi (44) mkazi wa kisasa Jijini hapa na Guard Abdala Ngola (59) ambaye ni mkazi wa Area c Dodoma.Akizungumza katika eneo la tukio, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema Treni hiyo ilikuwa ikitokea kigoma ,mwanza na mpanda kuelekea Dar es salaam ikiwa na behewa 9 za daraja tatu mbili za daraja kwanza,Behewa la mgahawa moja,Behea la vifurushi moja na Behea la Breki Moja na kusababisha majeruhi kwa abiria 32 waliokuwa kwenye Behewa namba 3648 na 3607 ambayo yalianguka.”Mnamo tarehe 17a ya 11/06/2019 majira ya saa 11:25 usiku ilianza safari kutoka Tabora kuelekea Dar es Salaam ikiwa na mabehewa 14 kama yalivyotajwa hapo juu na ilipofika maeneo ya kuvuka makutano ya Reli na kugongwa na gari”amesema MurotoMuroto amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari alipokuwa akivuka makutano ya Reli na barabara hivyo gari kuzima likiwa katikati ya Reli na Dereva wa gari aliruka na kukimbilia Polisi KujisalimishaAidha, kamanda muroto ameongeza kuwa hali ya abiria waliopata ajali hiyo kati ya abiria 32 watatu hali sio za kuridhisha.Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobasi katambi ameliomba jeshi la polisi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kujua chanzo cha ajali hiyo.