Home Michezo TANGA,LINDI KESHO KUFUNGUA DIMBA ROBO FAINALI SOKA WAVULANA UMISSETA

TANGA,LINDI KESHO KUFUNGUA DIMBA ROBO FAINALI SOKA WAVULANA UMISSETA

0

Wachezaji wa timu za mpira wa miguu wavulana kutoka mkoa wa Ruvuma (fulana ya bluu) wakichuana vikali na timu kutoka mkoa wa Dodoma jana katika hatua ya makundi ambapo Ruvuma waliwafunga Dodoma goli 1-0

Timu ya soka ya mkoa wa kilimanjaro wasichana wakimenyana na wenzao kutoka mkoa wa Morogoro katika hatua ya makundi ambapo Kilimanjaro iliibugiza Morogoro kwa magoli 7-0.

Patashika katika lango la timu ya soka wavulana ya mkoa wa Shinyanga wakati ilipopambana na wenzao kutoka mkoa wa Iringa ambapo shinyanga iliifunga Iringa goli 2-1

…………………

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Robo fainali ya soka kwa wavulana  inatarajia kuanza kesho katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara ambapo  miamba ya soka kutoka mikoa minane inatarajiwa kuonyeshana kazi katika  viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.

Mratibu wa mashindano ya UMISSETA Taifa bwana Leonard Thadeo amezitaja timu zilizofuzu hatua hiyo kuwa ni pamoja na Tanga, Lindi, Ruvuma, Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza, Songwe na Manyara.

Thadeo amesema kuwa mshindi wa kundi A ambaye ni Tanga atachuana na mshindi wa kundi C Lindi saa nane mchana na kufuatiwa na pambano kali kati ya mshindi kundi B mkoa wa Ruvuma ambao watachuana vikali na mshindi wa pili kundi D timu ya mkoa wa Kilimanjaro.

Katika mchezo mwingine wa robo fainali timu ya mkoa Mbeya ambao walikuwa washindi wa kwanza kundi C watachuana na mshindi wa pili kundi B ambao ni Mwanza, mechi ambayo itaanza saa 9.40 mchana, huku mechi nyingine ya robo fainali itawahusisha timu ya Songwe ambao ni washindi wa kwanza kundi D watameenyana na mshindi wa pili kundi A ambao ni Manyara.

Kwa upande wa soka wasichana, timu zilizofuzu hatua ya robo fainali ni Dar es salaam, Lindi, Iringa, Morogoro, Mwanza, Tabora, Kilimanjaro na Ruvuma.

Mechi za robo fainali kwa soka wasichana zilitarajiwa kuchezwa jioni ambapo timu ya mkoa wa Dar es salaam imepangwa kucheza na timu ya wasichana Lindi, timu ya mkoa wa Iringa imepangwa kumenyana na Morogoro, Mwanza itacheza naTabora, na Kilimanjaro wasichana itamenyana na timu kutoka mkoa wa Ruvuma.

Mechi za nusu fainali soka wavulana na wasichana zinatarajiwa kufanyika tarehe 19 juni 2019, wakati ambapo mechi za kutafuta mshindi wa tatu na fainali zinatarajiwa kufanyika tarehe 20 juni, 2019 katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara