*************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Juventus ya nchini Italia imemtangaza aliyekuwa kocha wa klabu ya Chelsea Maurizio Sarri kuwa kocha wao mpya atakaeiongoza klabu hiyo kwa msimu ujao.
Muitaliano huyo amejiunga na Juventus kwa mkataba wa miaka mitatu akichukua mikoba ya Massimiliano Allegri ambaye alitangaza kutundika daruga hivi karibuni.
Ikumbukwe kuwa kocha huyo ameiongoza klabu ya Chelsea kwa msimu mmoja na kuisaidia kunyakuwa taji la Ueropa league mbele ya mahasimu wao wa jiji moja Arsenal na pia kuisaidia klabu hiyo kushiriki michuano ya klabu Bingwa Ulaya kwa msimu ujao.
Chelsea watapata fidia ya £5M kutoka Juventus kutokana na dili hilo ambalo huenda likafungua milango kwa Frank Lampard kujiunga na Chelsea kama kocha mkuu.