Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Albert Jonkergouw akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 19 wa wanahisa wa Benki ya NMB uliofanyika jijini Dar es Salaam, jana
*********************************
Wanahisa wa Benki ya NMB wameidhinisha kiasi kilichopendekezwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM), uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Ikiwa ni matokeo ya utendaji bora na uimara wa nafasi ya mitaji, malipo ya jumla ya gawio la Shilingi Bilioni 33 (sawa na Shilingi 66 kwa kila hisa), yanafanana na sera ya benki ya kulipa moja ya tatu (asilimia 33.3) ya faida la jumla baada ya makato ya kodi (PAT) katika gawio. Hili ni ongezeko la asilimia 3 ukilinganisha na bei ya Shilingi 64 kwa kila hisa iliyolipwa mwaka uliopita.
Nia ni kukuza kiwango cha gawio kwa kila hisa, kulingana na utendaji bora wa benki unavyoongezeka.
Benki iliripoti faida ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 142 kabla ya makato ya kodi (PBT), kwa mwaaka wa fedha ulioishia Desemba 31 2018; ambayo ni ongezeko la asilimia 3 kutoka faida ya Shilingi Bilioni 138 iliyopatikana mwaka uliotangulia. Licha ya mafanikio yaliyopatikana, Bodi na Uongozi wa Benki ya NMB umeridhishwa na aina ya mafanikio na mapinduzi chanya katika
kipindi cha mwaka.
Mapinduzi hayo ni pamoja na uzinduzi wa NMB KLiK, mikopo ya mshahara – ambayo ni bidhaa ya kwanza ya benki kutoa mkopo kwa njia ya simu. Kuanzishwa kwa Mawakala zaidi ya 6800, wanaoshughulika – pamoja na mambo mengine, ukusanyaji na ulipaji wa kodi, ushuru na mapato ya Serikali za Mitaa katika Halmashauri 180, mapinduzi yanayochangia mzunguko wa pesa kwa mifumo ya kidijitali na kukuza amana. Pia tumeimarisha huduma za kibenki kupitia mtandao ilikuhudumia vizuri zaidi akaunti za makampuni na kuwapa suluhisho zote kamilifu na kufanya miamala ambayo imesababisha ongezeko la wateja kutoka milioni 2.2 hadi milioni 3.1 mwishoni wa mwaka 2018 .
Uimara wa NMB kama taasisi za fedha imepelekea Moody kuipa alama ya B1 ambayo vimethibitisha kuaminiwa kwa Benki ya NMB na wawekezaji wa kimataaifa. Benki imeimarishwa vema na uwiano wa mtaji kwa asilimia 16.5.Hiyo inamaanisha kwamba benki yetu iko salama kabisa kibiashara Mwenyekiti wa Benki, Prof. Joseph Semboja, anabainisha kuwa Bodi inataka kuweka sawa ongezeko la wanahisa, sambamba na kuimarisha biashara ya fedha
ndani ya benki katika mpango mkakati wa kukua zaidi kiuchumi.
“Kwa miaka kadhaa sasa NMB imeendelea kuwa imara yenye afya kifedha, lengo ni kuendelea kuimarika zaidi na kubaki hivyo. Ili kufikia mafanikio haya, tunapaswa kuhakikisha tunafanya maamuzi sahihi hasa katika udhibiti wa mabadiliko kwenye mahitaji makuu ya kimtaji,” anasema Mwenyekiti.
“NMB imejipambanua katika kuendelea kusaidia harakati za maendeleo ya uchumi Tanzania na kuvuka kiwango cha sasa cha dira ya uchumi kama kichocheo cha ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi nchini. Tutaendelea kuwa vinara wa hudumaa bora kwa wateja wetu, huku
tukiendelea kutimiza wajibu wetu kwa jamii,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Albert Jonkergouw.
NMB imejitolea katika kusaidia ukuaji kiuchumi wa wajasiriamali wadogo na wakati (SME's), hususani wanawake kwa kuwapa mafunzo na elimu ya uwezeshaji katika kuimarisha biashara zao kwa kutambulisha jukwaa jipya la ‘Woman in Banking’ kote nchini. Katika kilimo, NMB tumeboresha jopo la wataalamu wanaojikita zaidi katika Sekta ya KilimoBiashara, ili kuimarisha
mnyororo wa thamani unaopewa usaidizi mkubwa na Taasisi ya NMB Foundation, ambayo inatoa elimu katika Taasisi za Sekta ya Kilimo.
"Sisi ni Benki Bora Tanzania. Ubora wetu ni katika nyanja zote, za utawala, teknolojia ya habari na mfumo mzima unaoifanya NMB kuwa benki salama nchini, huku tukihakikisha amana na akiba zako ziko salama chini yetu," aliongeza.