Afisa Tarafa Mihambwe Ndg. Emmanuel Shilatu ameanza ziara ya kutembelea Kata kwa Kata kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za Wananchi akiambatana na Watendaji pamoja na wataalamu wa kata na Vijiji.
Katika mkutano wa Kwanza uliofanyika Kijiji cha Mkaha kilichopo kata ya Mihambwe Gavana Shilatu alitoa fursa kwa Watendaji na wataalamu hao kuelezea mafanikio ya Serikali yaliyopatikana kwenye maeneo yao na pia kujibu na kutoa ufafanuzi wa hoja za Wananchi.
Gavana Shilatu pia alitumia mkutano huo kuelezea mafanikio ya Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuliambapo mafanikio hayo yanavyowaguza moja kwa moja Wananchi wa maeneo ya vijijini.
Gavana Shilatu alisisitiza Watendaji na Wataalamu tubadilike kiutendaji ili kuendana na kasi ya kimaendeleo na kiutendaji aliyonayo Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kutekeleza ilani ya uchaguzi, kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.