Home Mchanganyiko Agizo la Jaffo Lawaamsha Usingizini Viongozi Arusha ,Watekeleza kwa kasi

Agizo la Jaffo Lawaamsha Usingizini Viongozi Arusha ,Watekeleza kwa kasi

0

Na Ahmed Mahmoud,Arusha

Serikali ya wilaya ya Arusha kwa kushirikiana na jiji la Arusha imeanza kutekeleza agizo la waziri wa nchi ofisi ya Rais, TAMISEMI,Suleiman Jaffo alilotaka  jengo la hospitali mpya ya Wilaya,ambalo ujenzi wake umekamikija ,kuanza kutoa Huduma Mara Moja  kwa wananchi.

Mei 25,mwaka huu waziri Jaffo alitembelea mradi wa jengo hilo uliopo eneo la Njiro Kontena jijini hapa na kukuta limekamilika muda mrefu lakini halifanyi Kazi ,ambapo alitoa wiki mbili kwa uongozi wa wilaya na halmashauri ya Jiji la Arusha kuhakikisha hospital hiyo inafunguliwa Mara Moja na kutoa Huduma kwa wananchi.

Akiongea na vyombo vya habari katika hospital hiyo Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqqar alisema hospitali hiyo tayari imeshaanza kutoa Huduma za chanjo na inatarajiwa kuanza kutoa Huduma zingine za matibabu muda mfupi ujao baada ya vifaa Tiba kuwasili.

Katika hatua nyingine  Dagarro alisema wilaya hiyo kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Arusha ,imeingia mkataba wa ujenzi wa jengo lingine la Mama na Mtoto linalojengwa katika hospitali hiyo na kampuni ya ukandarasi ya BQ Contractors LTD ya jijini Dar as salaam .

Alisema mradi huo utagharimu kiasi cha sh,Bilioni 1.36 fedha ambazo ni za ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha na utakamilika katika kipindi cha miezi saba kuanzia sasa.

“Leo tumekuja kumkabidhi ukandarasi ujenzi wa jengo la Matenet ambalo utenzi wake utachukua miezi saba kukamikika” alisema Daqqar

Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya  BQ ,Mhandisi John Bura alisema kuwa katika kipindi cha miezi saba ya Mkataba  watahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati katika kiwango kinachotakiwa.

“Tutahakikisha tunatekeleza mradi huu kwa viwango vya hali ya juu katika muda tuliokubaliana “Alisema Mhandisi Bura.

Awali Mkurugenzi wa jjji la Arusha,Dkt Maulid Madeni alisema  kuwa kuchelewa kufunguliwa kwa hospital ya wilaya ambayo ujenzi wake umekamilika kumetokana na kubadilika kwa matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kiasi cha sh,milioni 100.

Alisema sehemu ya fedha hizo,sh,milioni 70 zilitumika kujenga eneo la X Ray katika kituo cha Afya cha Muriet,huku fedha zingine kiasi cha sh, milioni 30 zikielekezwa katika umaliziaji wa ujenzi katika kituo cha Afya cha Kaloleni.

Aliongeza kuwa halmashauri hiyo tayari imeagiza vifaa Tiba kwa ajili ya hospital hiyo ya wilaya  kutoka bohari kuu ya dawa (MCD) na vinatarajiwa kufika Arusha mwezi ujao ,julai mwaka huu.

Naye Meya wa jiji la Arusha,Kalist Lazaro  amesema kuwa halmashauri hiyo imeelekeza ujenzi wa majengo ya juu (Gorofa) na wanatarajia kujenga majengo 10 katika hospital hiyo ya wilaya kwa ajili ya vitengo mbalimbali vya Tiba na Afya.

Alisema hatua hiyo ni kutokana na ufinyu wa maeneo ya wazi katika Jiji la Arusha na kupelekea halmashauri hiyo kujiwekea mkakati wa ujenzi wanyumba za gorofa.