Dkt. Analice Kamala akifafanua mada kwa wanahabari katika mafunzo ya usalama wa chakula ulioandaliwa na mamlaka ya chakula na dawa nchini tfda
Msemaji wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa habari walipo katika mafunzo ya usalama wa chakula ulioandaliwa na mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA
**************************
NA EMMANUEL MBATILO
Msemaji mkuu wa serikali Dkt. Hassan Abbasi ameziagiza taasisi za umma na idara za serikali kuweka programu za kuelimisha wana habari na vyombo vya habari ili kufikia malengo badala ya kutumia utamaduni wa kutoa adhabu pale ambapo waandishi wanakosea huku kukiwa hakuna jitihada za kuwapatia elimu za kitaasisi au kisekta.
Dkt. Abbasi amesema hayo mjini Bagamoyo mkoani Pwani wakati akizungumza na waandishi wa habari walipo katika mafunzo ya usalama wa chakula ulioandaliwa na mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kuwa serikali ya wamu ya tano inatambua na itaendelea kuilea taaluma ya habari kama kiungo muhimu baina ya wananchi na serikali kama ilivyo ridhia katika mikataba ya kimataifa miaka ya nyuma
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula (TFDA), Dkt. Candida Shirima amewapongeza wanahabari kwa kuitikia wito pamoja na kujitoa kwa moyo hasa katika kuhakikisha wanapata elimu kuhusu Chakula Salama na kuwafikishia wananchi taarifa zilizorasmi kuhusu usalama wa chakula.
Hata hivyo Kwa upande wa Afisa mwandamizi –Uchanganuzi wa hatari zitokanazo na chakula Dkt. Analice Kamala akiwasilisha mada yake katika semina hiyo amesema ulaji wa chakula kilichochafuliwa na kiasi kikubwa cha Sumukuvu husababisha madhara ya kiafya na hata kifo na hata hivyo madhara hayo huweza kujitokeza baada ya muda mfupi au mrefu kutegemea kiasi cha Sumukuvu kwenye chakula kilicholiwa, muda ambao chakula kilichochafuliwa kimekuwa kikitumika, umri wa mlaji na hali ya afya kwa ujumla.
“Madhara yanayotokea kwa muda mfupi hutokea baada ya mtu kula chakula kilichochafuliwa na sumukuvu kwa kiasi kikubwa na madhara hayo ni pamoja na kuathirika kwa ini, figona hata kifo”. Amesema Dkt.Analice.
Dk. Ameongeza kuwa Sumukuvu huweza kudhibitiwa kwenye mazao ya mahindi na karanga kabla ya kuvuna na baada ya kuvuna hasa wakati wa kuanika, usafirishaji, uhifadhi, utayarishaji na usindikaji.