Home Mchanganyiko WANANCHI WAPOKEA KWA MIKONO MIWILI MRADI WA UJENZI WA BANDARI YA KAREMA

WANANCHI WAPOKEA KWA MIKONO MIWILI MRADI WA UJENZI WA BANDARI YA KAREMA

0

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh. Saleh Mhando akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake  kuhusu mradi wa ujenzi wa bandari ya Karema.

…………………………………………………………………

Wananchi wa Karema wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wameupokea kwa mikono miwili mradi wa ujenzi wa Bandari ya Karema  utakaohusisha ujenzi wa Gati,Majengo , njia za Reli” (Wind Breakers) ndani ya bandari’.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh. Saleh Mhando amesema wananchi wa Karema wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Dkt.John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kujenga bandari hiyo.

“Sisi kama Wilaya ya Tanganyika pamoja na wananchi wote tunaunga mkono  Juhudi za Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi huu wa ujenzi wa mradi huo wa Bandari na tutashiriki kutoa mchango wetu wa hali na mali kwa asilimia 100% mpaka kukamilika kwa mradi huo ambao utakuwa ni ukombozi wa kiuchumi kwetu  pamoja na taifa kwa ujumla wake”

Mradi huo wa bandari ya Karema unatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 63 za kitanzania na mkandarasi yuko katika hatua za mwisho za matayarisho ya kuanza kwa ujenzi wa mradi huo.

Ameongeza kuwa wananchi wa wilaya ya Tanganyika ni wakulima wazuri wa mazao mbalimbali ya biasharaina na chakula, Lakini pia ni wavuvi wazuri hivyo mara bandari hii itakapokamilika itaamsha ari ya shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa wilaya ya Tanganyika.

 “Nina imani wananchi wengi watatumia fursa zitakazokuja kupitia bandari ya Karema kwa kusafirisha mazao yao kiurahisi kwenda na kutoka  maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi hivyo kuwaongezea kipato katika maisha yao ya  kila siku kiuchumi” Amesema Mhando.

Ameongeza kuwa bandari ya Karema itakapokamilika itaongeza  pato letu kiwilaya na taifa kwa ujumla kwa sababu mizigo mingi inayokwenda nchi jirani kama za DRC Congo, Burundi na Zambia itaweza kupitia bandari ya Karema, na kuongeza zaidi watumiaji wa Bandari yetu na Reli hivyo kukuza uchumi wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh. Saleh Mhando akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu mradi huo kushoto ni Mkurugenzi wa wilaya hiyo Bw. John Lomuli.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh. Saleh Mhando akisisitiza jambo wakati akizugumza na waandishi wa habari ofisini kwake.