Home Mchanganyiko UJENZI WASHIKA KASI … NI ULE GAVANA SHILATU ALIOAGIZA UJENGWE

UJENZI WASHIKA KASI … NI ULE GAVANA SHILATU ALIOAGIZA UJENGWE

0

*************************

Afisa Tarafa Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu ametembelea na kujionea ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa na chumba kimoja cha ofisi kwenye shule ya msingi Namunda iliyopo Kijiji cha Namunda kata ya Kitama ukiendelea kwa kasi tangu usimame Agosti, 2018.
Gavana Shilatu alijionea hayo kwenye ziara yake ya ufuatiliaji wa mradi huo wa ujenzi alioagiza ujengwe mara moja siku alipotembelea mradi huo Mei 16, 2019 kutokana na kutelekezwa tangu mwaka jana kwenye usawa wa ngazi ya msingi.
Gavana Shilatu aliwasisitizia uongozi wa Kijiji na kamati ya ujenzi kuacha malumbano ya wenyewe kwa wenyewe na wawe wazalendo kwa kuhakikisha wanathamini pesa ya umma na ujenzi uwe wenye ubora na viwango vinavyolingana na thamani ya pesa.
Katika ziara hiyo ya ufuatiliaji Gavana Shilatu aliambatana na uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Namunda pamoja na kamati ya ujenzi.