Home Michezo Michuano ya UMISSETA yaendelea Mtwara

Michuano ya UMISSETA yaendelea Mtwara

0

Mshambuliaji hatari wa timu ya soka wasichana ya Mkoa wa Kilimanjaro Siriel Jofrey “Messi” mwenye mpira akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya mkoa wa Morogoro katika mchezo baina ya timu hizo mbili hatua ya makundi uliochezwa leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara. Katika Mchezo huo timu ya mkoa wa Kilimanjaro iliibuka na ushindi mnono dhidi ya  Morogoro

Patashika katika mchezo wa volleyball baina ya timu za wasichana kutoka mikoa ya Pwani na Mara. Anayepiga mpira ni Salome Thomas wa Mara

Mshindi w a kwanza, pili na wa tatu katika mchezo wa riadha wa kupokezana vijiti mita mia 400 wasichana mara baada ya kukamilika kwa mbio hizo.

*********************

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Mashindano ya  Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (UMISSETA imeendelea leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara ambapo michezo mbalimbali imechezwa.

Jumla ya wanafunzi wa shule za sekondari wapatao  3304 kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara na miwili ya Zanzibar wanashiriki michezo hiyo

Kwa mujibu wa Mratibu wa Mashindano hayo bwana Leonard Thadeo michezo hiyo ipo katika hatua ya makundi ambapo yamegawanywa katika makundi manne

Katika michezo iliyochezwa jana kwa upande wa Netiboli

Geita 33 v/s Katavi 7

Shinyanga 21 v/s Songwe 16

Iringa 30 v/s Njombe 13

Mtwara 25 v/s Lindi 24

Pwani 03 v/s Kilimanjaro 26

Singida 13 v/s Mara 20

Mbeya 30 v/s Kagera 24

Mwanza 32 v/s Arusha 13

Dar  44 v/s Kigoma 14

Tanga 35 v/s Unguja 06

Morogoro 37 v/s Tabora 20

 Matokeo ya mchezo wa kikapu wavulana hatua ya makundi

Shinyanga  38 v/s Mwanza 32

Mara 10 v/s Unguja 48

Simiyu 26 v/s Rukwa 23

Ruvuma 19 v/s Njombe 20

Pemba 08 v/s Pwani 38

Kigoma 47 v/s Lindi 13

Morogoro 46 v/s Tabora 35

Iringa 25 v/s Singida 14

 Matokeo ya mchezo wa kikapu wasichana hatua ya makundi

Songwe 17 v/s Dodoma 21

Mtwara 24 v/s Lindi 12

Tanga 11 v/s Singida 12

Ruvuma 18 v/s Geita 25

Mwanza 34 v/s Iringa 07

Mara 05 v/s Arusha 16

Mtwara 17 v/s Kagera 10

Tabora 22 v/s Shinyanga 17

 Matokeo ya mchezo wa soka wavulana hatua ya makundi

Mtwara 0 v/s Singida 2

Iringa 1 v/s Arusha 1

Shinyanga 0 v/s Tanga 2

Ruvuma 1 v/s Mwanza 1

Unguja 2 v/s Morogoro 1

Rukwa 0 v/s Dodoma 1

Kigoma 0 v/s Mbeya 2

Pemba 0 v/s Lindi 3

Tabora 0 v/s Dar es salaam 1

Songwe 2 v/s Kagera 2

Njombe 1 v/s Simiyu 1

Geita 0 v/s Kilimanjaro 4

 

Matokeo ya mchezo wa soka wasichana hatua ya makundi

Ruvuma 2 v/s Mara 1

Dar 2 v/s Geita 0

Shinyanga 0 v/s  Iringa 2

Arusha 1 v/s Singida 2

Tabora 5 v/s Rukwa 1

Mwanza 8 v/s Mtwara 2

Njombe 0 v/s Mbeya 3

Morogoro 1 v/s Kagera 3

Manyara 1 v/s Katavi 2