Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisalimiana na kocha wa timu ya Polisi ya Zanzibar, Zuberi Ahmad mara baada ya kuzindua mashindano ya Kikapu ya Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Mwanza kabla ya mchuano kuanza kati ya timu hiyo ya Polisi na MTC ya Mwanza
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (wa pili kushoto) akisitiza jambo wakati akiangalia mpira wa kikapu kati ya timu ya Polisi Zanzibar na MTC ya Mwanza ambapo timu ya Polisi Zanzibar waliibuka washindi. Wa kwanza kushoto ni Meneja Masoko wa Jembe Fm, Domina Erasto na kulia ni Meneja wa Jembe FM , Fredy Kikoti.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa mpira wa wavu ya MTC Mwanza kabla ya kufungua mashindano ya wavu ya Afrika mashariki yanayofanyika jijini Mwanza
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa mpira wa wavu ya Polisi Zanzibar kabla ya kufungua mashindano ya wavu ya Afrika mashariki yanayofanyika jijini Mwanza
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia mtanange kati ya timu ya Polisi ya Zanzibar na MTC ya Mwanza mara baada ya mashindano hayo ya wavu ya Afrika Mashariki kufunguliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu katika viwanha vya Milongo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya MTC ya Mwanza wakati wa kufungua Mashindano ya wavu ya Afrika Mashariki kabla ya mechi kuanza kati ya timu ya MTC ya Mwanza na Polisi Zanzibar.
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa mpira wa wavu wakiwa wameshika bango wakiwa wanaelekea kwenye viwanja vya Milongo kwa ajili ya ufunguzi wa Mashindano ya wavu ya Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Mwanza.
( Picha zote na Lusungu Helela)
…………………
Serikali imeahidi kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mchezo wa wavu ambao ni miongoni mwa michezo iliyosahaulika licha ya kuwa ni mchezo wenye kuvutia watu wengi na unaweza kutumika kama sehemu ya watu kujiajiri
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati alipokuwa akifungua mashindano ya wavu ya Afrika Mashariki katika viwanja vya Milongo yajulikakanayo kwa jina la Jembe Mirjan East Africa Volleyball Championship yanayofanyika jijini Mwanza.
Mashindano hayo yana shirikisha timu sita na yatafanyika ndani ya muda nne ambapo mashindano hayo yameanza kati ya timu ya MTC Nyegezi dhidi ya Polisi Zanzibar ambapo mchezo umemalizika huku Zanzibar Polisi wakiongoza kwa goli 39 kwa 30
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Mhe.Kanyasu amewataka wachezaji wawe wavumilivu kutokana na changamoto wanazozipitia kwa vile mchezo wa wavu mbali na mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo ambao umekuwa ukikosa Wadhamini kwa sababu haujaweza kufahamika kiasi cha kuwashawishi Wadhamini kuweza kuweka pesa zao.
Amewaeleza wachezaji hao kuwa lazima wakubali kuumia kwanza kwa hiki kipindi cha mwanzo ili baadaye wadhamini waweze kujitokeza.
Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewahakikishia waandalizi wa mchezo huo kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro itadhamini mchezo huo kama ilivyokuwa imeahidi mwanzo
Naye, Meneja wa Jembe FM, Fredy Kikoti amesema mchezo huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi ikiwa pamoja na kukosekana kwa wadhamini hali iliyopelekea baadhi ya timu kushindwa kushiriki katika mashindano hayo.
Amesema mashindano hayo tangu yalipoanzishwa mwaka jana yamekuwa chanzo cha kuibua vipaji kwa vijana wa Kanda ya ziwa pamoja na Tanzania kwa
Ujumla
Mashindano hayo ya Afrika Mashariki yameanza Juni 12 mwaka huu yanatarajia kumalizika Juni 16 mwaka huu katika viwanja vya Milongo