Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayoub Ryoba (kushoto),
akiwa kwenye mazungumzo na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, wakati
meneja huyo alipotembelea studio za TBC Mikocheni jijini Dar es Salaam Juni 12,
2019. Ziara hiyo ilikuwa ni muendelezo wa ziara ya Bi. Chiume kutembelea vyombo
vya habari jijini ili kuimarisha mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo
ambao ni mpya. PSSSF iliundwa baada ya kuunganishwa kwa Mifuko minne ya Hifadhi
ya Jamii ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF. Vyombo vingine ambavyo PSSSF ilivitembelea katika ziara ya Juni 12, 2019 ni pamoja na Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL), Kampuni ya African Media Group, wamiliki wa Channel Ten na Magic FM, kampuni inayochapisha gazeti la Jamhuri, Kampuni ya New Habari (2006) wachapishaji wa magazeti la Mtanzania, Rai, na Dimba. Pamoja na mambo mengine, Meneja huyo kiongozi amesema Mfuko umeanza kutekeleza majukumu yake Agosti 1, 2018 na kwamba uko imara na kuwahimiza wastaafu wajitokeze kwa wingi katika zoezi la kuhakiki taarifa zao ili kuondoa usumbufu wakati wa kufanya malipo ya pensheni na kutoa hakikisho la kupata huduma bora na za haraka.
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume akizungumza wakati alipotembelea ofisi za New Habari Sinza jijini Dar es Salaam
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume akizungumza na uongozi wa kampuni ya New Habari Sinza jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Uhusiano Mwanzamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi na kulia kwake ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Denis Msacky.
Bi Eunice Chiume akipo ngozana na Mhariri wa gazeti la Jamhuri, Bw.