Home Michezo MAN UNITED KUANZA NA CHELSEA MSIMU MPYA LIGI KUU ENGLAND 2019/2020

MAN UNITED KUANZA NA CHELSEA MSIMU MPYA LIGI KUU ENGLAND 2019/2020

0

TIMU ya Manchester United na Chelsea zitakutana katika mchezo wa ugunguzi wa Ligi Kuu ya England  Uwanja wa Old Trafford Agosti 11 msimu ujao wa 2019-20, imeelezwa leo.
Msimu wa kwanza kamili wa Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wa Mashetani Wekundu utaanza kwa mchezo mgumu dhidi ya Chelsea ambayo itaanza maisha mapya bila Eden Hazard.
Tottenham pia itakuwa na mechi ngumu mwanzoni, washindi hao wa pili wa Ligi ya Mabingwa wakimenyana na Manchester City na Arsenal ugenini kwenye mechi zao nne za mwanzo.

Manchester United itafungua dimba na Chelsea msimu wa 2019-20 Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA