Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu mbele) akiwasili katika nyumba ya Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Yahaya Masare, ili kutatua malalamiko ya kodi ya Majengo katika Mtaa wa Uzunguni Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia) akitoa ufafanuzi wa kodi ya majengo kwa Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Yahaya Masare, alipofika kujionea hali halisi ya nyumba na bili aliyotakiwa kulipa ya Sh. 100,000, jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Yahaya Masare (katikati) na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Dodoma Bi. Kabula Mwemezi wakizungumza jambo.
Nyumba ya Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Yahaya Masare , iliyopo jijini Dodoma ambayo TRA walimtaka alipe Sh. 100,000 badala ya Sh. 10,000 jambo liliomfanya Mbunge huyo kufikisha malalamiko kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ambaye alilipatia ufumbuzi suala hilo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
……………………
Na Peter Haule, WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango amewataka Mameneja wa TRA wa mikoa na Wilaya nchini kote kusimamia vema ukusanyaji wa kodi za majengo na kuhakikisha kuwa viwango vinavyotozwa ni vile vilivyoko kisheria.
Dkt. Kijaji ametoa rai hiyo mjini Dodoma baada ya kupata malalamiko kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi Mheshimiwa Yahaya Masare, kwamba Mamlaka ya Mapato mkoani Dodoma imempelekea ankara ya kodi ya jengo na kumtaka alipe shilingi laki moja badala ya shilingi elfu 10 zilizoainishwa kisheria kwa majengo ya kawaida.
Dkt. Kijaji ambaye alifika kwenye makazi ya Mbunge huyo, katika Mtaa wa Uzunguni Jijini Dodoma, alibaini kutokuwa na mawasiliano ya kutosha kati ya TRA na wateja wake jambo lililosababisha malalamiko ya mteja huyo na kuagiza Mameneja wa TRA mikoa na wilaya kuhakikisha wanawafikia wateja badala ya kuwaachia kazi viongozi wa mitaa peke yao.
Cue in- Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Awali, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mhe. Yahaya Masare alimweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji kwamba alishitushwa na hatua ya TRA mkoa wa Dodoma kumpelekea ankara hiyo yenye kiwango kikubwa cha madai wakati anafahamu vema sheria ya kodi ya majengo iliyopitishwa bungeni imeainisha viwango vya kodi kwa kila jengo lililoko katika maeneo ya mijini na vijijini
Cue in- Yahaya Masare Mbunge wa Manyoni Magharibi
Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoa wa Dodoma Bi. Kabula Mwemezi, amekiri kuwepo kwa kasoro ya ankara waliyompatia Mbunge huyo na kujitetea kwamba hali hiyo ilitokana na taarifa walizonazo zinazohusu wateja wote wanaomiliki majengo na kwamba suala hilo limepatiwa ufumbuzi
Cue in – Bi. Kabla Mwemezi, Meneja wa TRA Dodoma
Bi Mwemezi aliwataka wateja wenye malalamiko kuhusu ankara walizo letewa kutoa taarifa kabla hawajalipa ili waweze kupatiwa suluhisho.