Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiongozana na Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille wakati wakiingia katika hafla ya chakula cha jioni nyumbani kwa Spika Ndugai kisasa Jijini Dodoma. Kulia nyuma ni Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura na Mbunge ni Mbunge wa kasulu Mhe. Daniel Nswanzugwako
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na ugeni kutoka Bunge la Rwanda ulioongozwa na Spika wa Bunge hilo, Waheshimiwa Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge na wageni waalikwa waliofika katika hafla ya chakula jioni nyumbani kwake kisasa Jijini Dodoma. Wageni hao kutoka Bunge la Rwanda walifika nchini Tanzania kwa ajili ya kuboresha mahusiano baina ya Mabunge na nchini hizi mbili
Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille akizungumza na Waheshimiwa Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge na wageni waalikwa (hawapo kwenye picha) katika hafla ya chakula jioni nyumbani kwa Spika Ndugai kisasa Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kuboresha mahusiano baina ya Mabunge na nchini hizi mbili
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa tatu kulia), Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille (wanne kulia), Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura (wa pili kulia), Mbunge wa Kasulu, Mhe. Daniel Nswanzugwako (kulia), Mbunge wa Ngara, Mhe. Alex Gashaza (kushoto) na Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatma Mganga wakiwa katika hafla ya chakula jioni nyumbani kwa Spika Ndugai kisasa Jijini Dodoma.
Waheshimiwa Mawaziri, Manaibu Waziri na Wabunge wakiwa katika hafla ya chakula jioni nyumbani kwake kisasa Jijini Dodoma. Hafla ikiwa ni baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Rwanda uku dhumuni likiwa kuboresha mahusiano baina ya Mabunge na nchini hizi mbili
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akishuhudia Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akipatiwa zawadi na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge la Rwanda ya Masuala ya Siasa na Jinsia, Mhe. Rubagumya Emma wakati wa hafla ya chakula cha jioni nyumbani kwa Spika Ndugai kisasa Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akishuhudia Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (katikati) akipatiwa zawadi na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura wakati wa hafla ya chakula cha jioni nyumbani kwa Spika Ndugai kisasa Jijini Dodoma.