Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

0

Mnamo tarehe 10/06/2019 majira ya saa 08:50 asubuhi huko maeneo yam lima Yasini katika Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Chunya – Makongorosi  gari lenye namba za usajili T489 AUG aina ya scania, basi la abiria linalomilikiwa na Kampuni ya Sasebosa likiendeshwa na dereva SELEMAN S/O SALEHE miaka 48, mkazi wa Tabora ambaye alitoroka baada ya ajali, lilipinduka na kusababisha majeruhi kwa abiria wawili (02) ambao ni TILA D/O MBEYU , umri miaka 70, mkulima wa Dsm aliumia sehemu ya kiunoni, na wa pili ni  JANE D/O DAMIANI miaka 28, mkulima wa Kibaoni Chunya, aliumia sehemu ya kifuani na mkono wa kushoto na wote wawili walikimbizwa hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya kwa matibabu.

Chanzo cha ajali  bado kinachunguzwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi SEBASTIAN M. MBUTA anatoa wito  kwa madereva wa mabasi ya abiria na vyombo vingine vya moto wanatakiwa kuwa makini kufuata sheria za usalama barabarani muda wote wanapokuwa barabarani. Vilevile wamiliki wa magari wakishirikiana na madereva wao wanatakiwa kuhakikisha magari yao yanafanyiwa matengenezo (service) mara kwa mara kabla ya kuanza safari.

Vile vile rai kwa abiria pindi wanapokuwa safarini wanapobaini viashiria vya madereva kundesha mabasi ya abiria kwa mwendo kasi watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa hatua za haraka.

Mnamo tarehe 28/05/2019 majira ya asubuhi askari Polisi namba H. 9946 Pc Daniel wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kyela alitakiwa kuingia kazini lakini hakuingia na baada ya kufuatilia tulibaini kuwa ametoroka baada ya kutuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya Sekondaji ya Kyela anayesoma kidato cha kwanza.Juhudi za kumtafuta askari huyo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe  zinaendelea.

Aidha nasisitiza utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu kupitia namba za simu zifuatazo:-

RPC…………………………………………………………….0715 009 931

RCO…………………………………………………………… 0658 376 052

STAFF OFFICER…………………………………………….0658 376 006

OPERATION OFFICER……………………………………..0754 466 924

RTO…………………………………………………………….0658 376 472

OC FFU…………………………………………………………0658 376 009

OCD MBEYA…………………………………………………0659 884 996

OCD MBALIZI………………………………………………..0655 248 381

OCD CHUNYA……………………………………………….0655 248 381

OCD MBARALI………………………………………………0659 885 948

OCD RUNGWE………………………………………………0659 885 253

OCD KYELA…………………………………………………0659 887 919

Imetolewa na:

[SEBASTIAN M.MBUTA – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.