Mnamo tarehe 10/06/2019 majira ya saa 08:50 asubuhi huko maeneo yam lima Yasini katika Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Chunya – Makongorosi gari lenye namba za usajili T489 AUG aina ya scania, basi la abiria linalomilikiwa na Kampuni ya Sasebosa likiendeshwa na dereva SELEMAN S/O SALEHE miaka 48, mkazi wa Tabora ambaye alitoroka baada ya ajali, lilipinduka na kusababisha majeruhi kwa abiria wawili (02) ambao ni TILA D/O MBEYU , umri miaka 70, mkulima wa Dsm aliumia sehemu ya kiunoni, na wa pili ni JANE D/O DAMIANI miaka 28, mkulima wa Kibaoni Chunya, aliumia sehemu ya kifuani na mkono wa kushoto na wote wawili walikimbizwa hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya kwa matibabu.
Chanzo cha ajali bado kinachunguzwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi SEBASTIAN M. MBUTA anatoa wito kwa madereva wa mabasi ya abiria na vyombo vingine vya moto wanatakiwa kuwa makini kufuata sheria za usalama barabarani muda wote wanapokuwa barabarani. Vilevile wamiliki wa magari wakishirikiana na madereva wao wanatakiwa kuhakikisha magari yao yanafanyiwa matengenezo (service) mara kwa mara kabla ya kuanza safari.
Vile vile rai kwa abiria pindi wanapokuwa safarini wanapobaini viashiria vya madereva kundesha mabasi ya abiria kwa mwendo kasi watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa hatua za haraka.
Mnamo tarehe 28/05/2019 majira ya asubuhi askari Polisi namba H. 9946 Pc Daniel wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kyela alitakiwa kuingia kazini lakini hakuingia na baada ya kufuatilia tulibaini kuwa ametoroka baada ya kutuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya Sekondaji ya Kyela anayesoma kidato cha kwanza.Juhudi za kumtafuta askari huyo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe zinaendelea.
Aidha nasisitiza utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu kupitia namba za simu zifuatazo:-
RPC…………………………………………………………….0715 009 931
RCO…………………………………………………………… 0658 376 052
STAFF OFFICER…………………………………………….0658 376 006
OPERATION OFFICER……………………………………..0754 466 924
RTO…………………………………………………………….0658 376 472
OC FFU…………………………………………………………0658 376 009
OCD MBEYA…………………………………………………0659 884 996
OCD MBALIZI………………………………………………..0655 248 381
OCD CHUNYA……………………………………………….0655 248 381
OCD MBARALI………………………………………………0659 885 948
OCD RUNGWE………………………………………………0659 885 253
OCD KYELA…………………………………………………0659 887 919
Imetolewa na:
[SEBASTIAN M.MBUTA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Mnamo tarehe 10/06/2019 majira ya saa 08:50 asubuhi huko maeneo yam lima Yasini katika Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Chunya – Makongorosi gari lenye namba za usajili T489 AUG aina ya scania, basi la abiria linalomilikiwa na Kampuni ya Sasebosa likiendeshwa na dereva SELEMAN S/O SALEHE miaka 48, mkazi wa Tabora ambaye alitoroka baada ya ajali, lilipinduka na kusababisha majeruhi kwa abiria wawili (02) ambao ni TILA D/O MBEYU , umri miaka 70, mkulima wa Dsm aliumia sehemu ya kiunoni, na wa pili ni JANE D/O DAMIANI miaka 28, mkulima wa Kibaoni Chunya, aliumia sehemu ya kifuani na mkono wa kushoto na wote wawili walikimbizwa hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya kwa matibabu.Chanzo cha ajali bado kinachunguzwa.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi SEBASTIAN M. MBUTA anatoa wito kwa madereva wa mabasi ya abiria na vyombo vingine vya moto wanatakiwa kuwa makini kufuata sheria za usalama barabarani muda wote wanapokuwa barabarani. Vilevile wamiliki wa magari wakishirikiana na madereva wao wanatakiwa kuhakikisha magari yao yanafanyiwa matengenezo (service) mara kwa mara kabla ya kuanza safari.Vile vile rai kwa abiria pindi wanapokuwa safarini wanapobaini viashiria vya madereva kundesha mabasi ya abiria kwa mwendo kasi watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa hatua za haraka.Mnamo tarehe 28/05/2019 majira ya asubuhi askari Polisi namba H. 9946 Pc Daniel wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kyela alitakiwa kuingia kazini lakini hakuingia na baada ya kufuatilia tulibaini kuwa ametoroka baada ya kutuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya Sekondaji ya Kyela anayesoma kidato cha kwanza.Juhudi za kumtafuta askari huyo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe zinaendelea.Aidha nasisitiza utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu kupitia namba za simu zifuatazo:-RPC…………………………………………………………….0715 009 931RCO…………………………………………………………… 0658 376 052STAFF OFFICER…………………………………………….0658 376 006OPERATION OFFICER……………………………………..0754 466 924RTO…………………………………………………………….0658 376 472OC FFU…………………………………………………………0658 376 009OCD MBEYA…………………………………………………0659 884 996OCD MBALIZI………………………………………………..0655 248 381OCD CHUNYA……………………………………………….0655 248 381OCD MBARALI………………………………………………0659 885 948OCD RUNGWE………………………………………………0659 885 253OCD KYELA…………………………………………………0659 887 919Imetolewa na:[SEBASTIAN M.MBUTA – ACP]KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.