NJOMBE
Mwenyekiti wa kijiji cha Lupalilo wilayani Makete mkoani Njombe Method Pele ametishia kuachia madaraka kwa madai ya kwamba majukumu yamekuwa yakimzidia kwasababu mtendaji wa kijiji hicho amekuwa hakai katika kituo chake cha kazi kwa muda mrefu bila ya kuwa na sababu za msingi.
Amesema kwa muda mrefu amekuwa akifanya kazi zinazopaswa kufanywa na mtendaji jambo ambalo linadaiwa kukwamisha shughuli za maendeleo ikiwe kusimama kwa zoezi la ujenzi wa shule ya msingi ambao fedha za michango amekuwa akiondoka nazo na kukaa muda mrefu njee ya kituo na kuiomba serikali kumchukulia hatua mtumishi huyo.
Nao baadhi ya wananchi wakilalamikia hali hiyo akiwemo Supa Sanga na Amina John wamesema jambo la kushangaza kwa mtendaji huyo ambaye hakai kituoni amekuwa akichangisha fedha na kwenda nazo nyumbani kwake licha ya kumtaka kupeleka kwa mwalimu mkuu pindi anaposafiri jambo ambalo limemfanya kumuazimia katika mkutano wa hadhara.
Aidha wakazi hao wamesema kuwa kijiji chao kimekwama kabisa katika suala la maendeleo tangu mtumishi huyo afike kituoni hapo
Akitoa utetezi kuhusu tuhuma zinazo mkabili mtendaji huyo wa kijiji Katiba Mgaya amesema anashangazwa na malalamiko yanayotolewa na wananchi kwa kuwa hausiki na ujenzi wa majengo hayo bali jukumu lake ni kukusanya michango kama walivyokubaliana na kumua kukabidhi kiasi cha shilingi laki tatu na ishirini kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Lupaloli ambazo alikuwa amekusanya kwa wananchi.