Home Mchanganyiko MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI UNAOISHIA MEI WAPANDA

MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI UNAOISHIA MEI WAPANDA

0

Mkurugenzi wa shughuri za kitakwimu, kutoka ofisi ya taifa ya takwimu, Irenius Ruyobya, akitoa taarifa kwa wanahabari (hawapopichani), juu ya hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi unaoishia mei, 2019.

………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

OFISI ya taifa ya takwimu (NBS), imesema hali  ya mfumuko wa bei kwa mwezi ulioishia mei, 2019,  umepanda kwa asilimia 0.3 hadi kufikia 3.5 ukilinganishwa na ya mwezi april iliyokuwa 3.2.

Akisoma taarifa ya hali mfumuko wa bei kwa mwezi unaoishia mei, 2019, kwa  waandishi wa habari Jijini Dodoma Mkurugenzi wa shughuri za kitakwimu, kutoka ofisi  ya taifa ya takwimu Irenius Ruyobya amezitaja bidha zilizochangia kupanda kwa mfumuko wa bei kwa mwezi ulioishia mei.

Na kusababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 2.8, nyama kwa asilimia 4.7, samaki asilimia 13.5, matunda kwa asilimia 15.3, viazi kwa asilimia 21.7 na mihogo mibichi kwa asilimia 24.8.

“kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia  mwezi mei, 2019 kumechangiwa na  kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi mei, 2019 zikilinganishwa na bei za mwaka ulioishia mei,  2018”

“Baadhi ya bidhaa zilizochangia kupanda kwa mfumuko wa bei kwa mwezi ulioishia mei 2019, ni kwa bei za bidhaa za vyakula kama unga wa mahindi kwa asilimia 2.8, nyama kwa asilimia 4.7, samaki asilimia 13.5, matunda kwa asilimia 15.3, viazi kwa asilimia 21.7 na mihogo mibichi kwa asilimia 24.8” amesema Ruyobya.

Pia amezitaja baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa taifa ni pamoja na mavazi na viatu kwa asilimia 3.7, mkaa kwa asilimia 13.1, vyombo vya jikoni kwa asilimia 2.5, gharama za kumuona daktari hospitali za binafsi kwa asilimia 6.4, dizeli kwa asilimia 11.1 na petrol kwa asilimia4.2.

Kwa upande wa mfumuko kwa bidhaa  za vyakula na vinywaji baridi umeongezeka  hadi kufikia asilimia 2.2 kutoka asilimia 0.9 ya mwezi ulioishia april.

Amebainisha kuwa kwa upande wa mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika mashariki kwa mwezi ulioishia mei, 2019, Uganda umepungua kwa asilimia 0.2 kutoka 3.5 hadi kufikia 3.3.

Na kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei umepungua pia kwa asilimia 1.09 , kutoka asilimia 6.58 hadi kufikia asilimia 5.49, ukilinganisha na kipindi kilichoishia  mwezi april, 2019.

Ofisi ya taifa ya takwimu(NBS) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa sheria ya takwimu ya mwaka 2015 pamoja na mapitio yake ya mwaka 2018, ofisi ya takwimu ina mamlaka ya kutoa na kusimamia na kuratibu upatikanaji wa taarifa za kitakwimu nchini.