Home Mchanganyiko AFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA JIWE NA MWENZAKE-WANKYO

AFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA JIWE NA MWENZAKE-WANKYO

0

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

RASHID Said ( 17 )amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa jiwe lililompata kichwani eneo la kisogoni na mwenzake ambae ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Nyumbu huko Kibaha mkoani Pwani.

Kufuatia kutokea kwa tukio hilo, jeshi la polisi mkoani Pwani,linamshikilia mwanafunzi huyo ili kuendelea na taratibu za kisheria.

Kamanda wa polisi mkoani humo ,Wankyo Nyigesa aliwaambia waandishi wa habari kwamba,chanzo ni ugomvi uliotokea baina ya vijana hao.

Alieleza,,juni 7 mwaka huu maeneo ya Pichandege marehemu alijeruhiwa kwa kupigwa jiwe baada ya tukio hilo alipelekwa katika hospital ya rufaa ya Tumbi kwa matibabu ambapo juni 8 alifariki dunia.

“Mtuhumiwa siku ya tukio alikuwa akirudi nyumbani na alikutana na vijana wenzake akiwemo marehemu wakimzuia asipite na ndipo marehemu alianza kumtukana mtuhumiwa “

Wankyo alieleza,mtuhumiwa alifanya jitihada za kukimbia lakini kabla hajafika mbali marehemu alimrushia jiwe lililompiga ubavuni hivyo mtuhumiwa kuamua kumrushia jiwe marehemu lililompata kichwani kisogoni.

Mwili wa marehemu umepelekwa hospital ya taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi .

Jeshi la polisi Pwani linatoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kujiepusha na matatizo ama kujikuta wakichukuliwa hatua za kisheria.