*********************************
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt.Agnes Kijazi yupo nchini Uswisi –Geneva kwenye Mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-18 Congress) .Mkutano huu hufanyika kila baada ya miaka 4 ambapo mwaka huu unafanyika jijiji Geneva kuanzia tarehe 3- 14 juni ,2019.
Katika Mkutano huo utafanyika uchaguzi wa viongozi wakuu wa WMO ,ambao ni pamoja na Rais ,Makamu wa Kwanza wa Rais ,Makamu wa Pili wa Rais ,Makamu wa Tatu wa Rais na viongozi wengine wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO).
Tanzania kupitia Dkt Agnes Kijazi amejitosa katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya makamu wa tatu wa Rais wa WMO. Dkt Kijazi anaungwa mkono na wakuu wote wa taasis za hali ya hewa barani Afrika na azimio hili lilipitishwa katika Mkutano wa Mawaziri wenye Dhamana ya Huduma ya Hali ya Hewa Barani Afrika (African Ministerial Conference on Meterology – AMCOMET) tarehe18 – 23 F