Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Shinyanga inayojengwa katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mhe. Azza ametembelea hospitali hiyo Juni 7,2019 na kueleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa majengo nane ya kisasa katika hospitali hiyo unaotarajiwa kukamilika ifikapo Juni 30 mwaka huu.
“Niwapongeze sana kwa kasi hii ya ujenzi mnayoendelea nayo,nakuomba Mhe. Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga uweke mkazo zaidi ili kuhakikisha ujenzi huu ulioanza Januari mwaka huu,ukamilike Juni 30,2019 kama ilivyopangwa”,alisema Azza.
“Nitumie fursa hii kuipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Jemedari wetu, Rais wetu mpendwa, Dkt. John Pombe Magufuli kutupatia shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hii na na ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya Ushetu (Sh.Bilioni 1.5) mkoani Shinyanga ili kuwasogezea karibu huduma ya afya wananchi”,aliongeza Azza.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba alisema halmashauri yake ni miongoni mwa halmashauri 67 nchini zilizotengewa pesa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa hospitali huku akibainisha kuwa kutokana na kasi nzuri ya ujenzi wanayoendelea nayo ujenzi utakamilika ifikapo Juni 30.
Aliyataja majengo 8 yanayojengwa katika hospitali hiyo kuwa ni jengo la wazazi,wagonjwa wa nje,mionzi,maabara,kufulia,stoo ya dawa,kuhifadhia maiti na jengo la kuhifadhia dawa za chanjo.
ANGALIA PICHA
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (katikati) akiwasili katika hospitali ya wilaya ya Shinyanga inayojengwa katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kujionea jinsi ujenzi unavyoendelea. Kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (katikati) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Shinyanga inayojengwa katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kujionea jinsi ujenzi unavyoendelea. Mbele ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba.
Kushoto ni Msimamizi wa ujenzi katika hospitali ya wilaya ya Shinyanga,Willium John Lusiu akimweleza jambo Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad.
Msimamizi wa ujenzi katika hospitali ya wilaya ya Shinyanga,Willium John Lusiu akiendelea kumtembeza Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (kushoto) katika hospitali ya wilaya ya Shinyanga. Kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiangalia majengo yanayoendelea kujengwa katika hospitali ya wilaya ya Shinyanga.
Sehemu ya majengo yanayoendelea kujengwa katika hospitali ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiingia katika jengo la wodi ya wazazi.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba wakiwa katika jengo la wodi ya wazazi.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiangalia majengo yanayoendelea kujengwa katika hospitali ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiondoka baada ya kutembelea hospitali ya wilaya ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog