Home Biashara BANDARI NYINGI ZA ZIWA VICTORIA ZAUNGANISHWA NA MFUMO WA KIELEKTRONI ILI KUKUSANYA...

BANDARI NYINGI ZA ZIWA VICTORIA ZAUNGANISHWA NA MFUMO WA KIELEKTRONI ILI KUKUSANYA MAPATO KWA UFANISI

0

Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Geofrey Lwesya akiwaelezea waandishi wa habari utekelezaji wa mradi wa  ukarabati wa jengo la abiria na ofisi katika  Bandari ya Bukoba  wakati akifanya majumuisho ya ziara ya waandishi wa habari walipotembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika bandari za ziwa Victoria zinzosimamiwa na Mamlaka hiyo leo mjini Bukoba.

……………………………………………….

NA JOHN BUKUKU-BUKOBA

Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Geofrey Lwesya amesema ukarabati wa jengo la abiria katika Bandari ya Bukoba umefikia 95% ya utekelezaji wake. Mradi huu unategemewa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho tarehe 15.6.2019 na umegharimu kiasi cha shilingi milioni 143,856,160.00.

Akizungumza wakati alipokuwa akifanya majumuisho ya zaiara ya waandishi wa habari katika miradi ya bandari za ziwa Victoria  inayotekelezwa na serikali amesema kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa miradi hiyo unaenda vizuri na miradi mingi  imekamilika kwa wakati na iliyobaki pia itakamilikwa kwa wakati.

Lwesya ameongeza kuwa Bandari nyingi za Tanzania zimejengwa na zinaendelea kujengwa katika viwango bora na vya kisasa ukilinganisha na bandari za wenzetu ili kuendana na kasi ya kuhudumia wateja kwa ufanisi zaidi 

“Katika kuhakikisha mapato ya serikali yanakusanywa kikamilifu   bandari za Mamlaka zimeshaunganishwa na mfumo wa makusanyo ya mapato kwa njia ya kielektroniki na zilizobaki zinaendelea kuunganishwa “. Ameongeza Lwesya.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa uhusiano wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar Bi. Shamsa Mohamed amesema huduma wanazopewa na bandari  wanapo safirisha au kupokea mizigo  ni nzuri

Alisisitiza kwamba huduma hizo kwa sasa zimeboreshwa na kuwa zenye ufanisi zaidi kwa kuwa hutolewa  masaa 24.

” Tangu tuanze kutumia usafiri wa majini tumegundua kwamba una unafuu mkubwa na tunasafirisha bidhaa zetu kwa wingi ukilinganisha na usafiri wa barabara”

Mkuu wa uhusiano wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar Shamsa Mohamed akizungumza na waandishi wa habari katika bandari ya Bukoba kuhusu huduma wanayopewa na bandari ya Bukoba wanapo safirisha mizigo na kupokea bandarini hapo.

Muonekana wa jengo mara baada ya kukarabatiwa, jengo hili lilijengwa mwaka 1945.

Nahodha wa meli ya Luxury inayosambaza bia za TBL visiwani katika ziwa Victoria Kampten Peter Hiza akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati alipokuwa akizungumzia huduma za Bandari ya Bukoba leo.

Meli ya MV Luxury inayofanya safari zake katika ziwa victoria ikiwa katika bandari ya Bukoba.

Mzigo wa bia ukiwa tarai umeshushwa kwa ajili ya kupakiwa kwenye magari na kupelekwa katika maghala ya Bukoba.

Waandishi Khaleed Gangana wa TBC na Esther Mbusi wa Mtanzania wakifanya mahojiano na Shamsa Mohamed Mkuu wa Mawasiliano Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar.

Muonekano wa ndani wa jengo la kupumzikia abiria mjini bukoba hata hivyo jengo hilo bado halijaanza kutumika kwakuwa liko katika hatua za mwisho za ukarabati.

Moja ya viti vya kisasa vitakavyowekwa katika chumba cha abiria likoneshwa na Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Geofrey Lwesya leo.