Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwezeshaji wa AZAKI,Bw. Francis Kiwanga,akitoa taarifa kwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa wakati wa mkutano na Wakurugenzi wa Asasi pamoja na zoezi la kusaini mikataba ya Ruzuku kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi Tanzania bara na Visiwani Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara,akitoa hotuba katika Mkutano wa Wakurugenzi wa AZAKI na Zoezi la kusaini Mikataba ya Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Tanzania bara na Visiwani katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal Vilalage Hotel leo jijini Dodoma
Sehemu ya Wakurugenzi wa AZAKI wakifuatilia Hotuba ya Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara,wakati wa Mkutano wa Wakurugenzi wa AZAKI na Zoezi la kusaini Mikataba ya Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Tanzania bara na Visiwani katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal Vilalage Hotel leo jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara,akikata utepe wa kuashiria ufunguzi wa Mkutano wa Wakurugenzi wa AZAKI na Zoezi la kusaini Mikataba ya Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Tanzania bara na Visiwani katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal Vilalage Hotel leo jijini Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwezeshaji wa AZAKI, Bw.Francis Kiwanga akisimamia baadhi ya wadau wa AZAKI Zoezi la kusaini Mikataba ya Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Tanzania bara na Visiwani katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal Vilalage Hotel leo jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tusonge kutoka Moshi Bi.Aginata Rutazaa,akitoa shukrani kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara,mara baada ya kuwafungulia Mkutano wa Wakurugenzi wa AZAKI na Zoezi la kusaini Mikataba ya Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Tanzania bara na Visiwani katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal Vilalage Hotel leo jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara,akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki na viongozi wa AZAKI baada ya kufungua Mkutano wa Wakurugenzi wa AZAKI na Zoezi la kusaini Mikataba ya Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Tanzania bara na Visiwani katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal Vilalage Hotel leo jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog,Dodoma
………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mwita Waitara, amezitaka asasi za kiraia AZAKI, kuhakikisha zinaweka mifumo mizuri ya kusimamia fedha za miradi ili kuhakikisha zinawanufaisha wahitaji.
Sambamba na hilo amezitaka kufanya kazi kwa ukaribu na maafisa wa serikali za mitaa kwenye maeneo yanayotekeleza majukumu yao na kutoa taarifa kwa halmashauri ambako miradi hiyo inatekelezwa.
Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa mkutano na Wakurugenzi wa Asasi hizo, na zoezi la kusaini mikataba ya Ruzuku kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi Tanzania bara na Visiwani.
Amesema wahakikishe wanaweka mifumo mizuri ya usimamizi sahihi wa fedha za miradi wanayoitekeleza na kuhakikisha wahusika wananufaika na wanafikiwa kufikiwa na miradi hiyo.
“Niwaombe sana hakikisheni mnafanya matumizi sahihi ya fedha za miradi hii mnayoitekeleza na kuhakikisha wanafuika halisi wanafikiwa na kufaidika na miradi hiyo, poa mhakikishe mnawahusisha maafisa wa serikali za mitaa kwenye maeneo ya utekelezaji” amesema Waitara.
Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na asasi za kiraia katika kusukuma mbele maendeleo vijijini, kuleta teknologia mpya na rahisi kwa wananchi na kupinga mila potofu na kandamizi miongoni mwa jamii hasa maeneo ya pembezoni.
Amezitaka AZAKI zinapojenga uwezo kwa wananchi wajenge pia uwezo kwa viongozi wa serikali za mitaa ili wajue na kutekeleza majukumu yao kiufanisi kwa kupitia mafunzo mbalimbali katika miradi hii kwa pamoja washirikiane katika kutayua changamoto zilizopo.
Aidha amewataka AZAKI kutoa elimu kwa vijana juu ya mikopo ya vikundi inayotolewa na serikali ili waweze kunufaika, amesema imekuwa ikitolewa lakini vijana hawajitokezi kuchukua mikopo hiyo na kuwaacha akina mama wakinufaika na mikopo hiyo.
Akizungumzia ruzuku kwa mwaka huu Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya uwezeshaji wa AZAKI, Francis Kiwanga amesema kwa mwaka huu watatoa kiasi cha shilingi Bilioni 11.7, kwa asasi za kiraia 154 ambazo zimekidhi vigezo vya kupata ruzuku hiyo ili wakatekeleze majukumu yao.
Amesema madhumuni ya Taasisi hiyo ni kuwekeza katika utoaji wa ruzuku kwa AZAKI na kuleta mabadiliko chanya yanayogusa maisha ya watanzania kupitia AZAKI zao.
“Lengo hasa uwekezaji huu ni kuwajengea uwezo wananchi kupitia AZAKI na nafasi kubwa tunatoa kwa asasi kutoka ngazi za chini kabisa ya jamii ambapo wananchi wanabainisha matatizo yao na kupendekeza utatuzi sisi tunawapatia nguvu ya ruzuku na pia kuwajengea uwezo kupitia AZAKI” amesema Kiwanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya Tusonge kutoka Moshi, Bi Aginata Rutazaa, amesema wao kama asasi za kiraia watahakikisha wanaweka uwazi katika matumizi ya fedha hizo ili ziweze kuleta tija kwa wahusika.