Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa ameongoza Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam na Katibu Tawala wa mkoa huo leo wamefanya operesheni ya ukaguzi na matumizi ya vitambulisho vya wamachinga kwenye soko la Kariakoo na kubaini uwepo wa ukiukwaji mkubwa wa matumizi ya vitambulisho hivyo.
Katika ziara hiyo RC Makonda amebaini mambo matano ikiwemo Wafanyabiashara kufoji vitambulisho, wafanyabiashara kuazimishana vitambulisho, wafanyabiashara kukodi vitambulisho kwa shilingi 1,000, utofauti wa jina linalotumika kwenye kitambulisho kutofautiana na jina analotumia kwenye vitambulisho vingine pamoja na uwepo wa idadi kubwa ya wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho.
Kutokana na hayo RC Makonda amewaagiza wakuu wa Wilaya kuanza msako Mara moja wa kuwakamata wafanyabiashara waliofoji vitambulisho na wasiokuwa na vitambulisho iliwaweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Hata hivyo RC Makonda amesema ataandika barua ya Kumuomba Rais Dkt.John Magufuli amuongezee vitambulisho vingine 25,000 na kufanya mkoa huo kuwa na idadi ya vitambulisho 200,000