MKUUA MAFUNZO NA UTENDAJI KIVITA WA JWTZ MEJA JENERALI ALFRED KAPINGA AMBAYE ATAKUWA MGENI RASMI PAMBANO LA NGUMI JUNI SABA KATIKA UKUMBI WA 361 MWENGE JIJINI DAR ES SALAAM. PICHA KWA HISAINI YA JWTZ)
Na Dar es Salaam
Mkuu wa Mafunzo na Utendaji kivita wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Afred Kapinga anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika pambano la Ngumi za Kulipwa na Ngumi za wazi linalotarajiwa kufanyika Juni Saba katika Klabu ya Jeshi ya 361 Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mmoja wa Waratibu wa Pambano hilo lisilola ubingwa Beatrice Ntahona alisema Maandalizi yote yamekamilika ikiwemo hali za Mabondia na kinachosubiriwa ni mchezo mzuri huku mashabiki wakiangalia mpambano mzuri.
Tumemualika Meja Jenerali Kapinga kutoja JWTZ kwanza ndie msimamizi mkuu wa masuala ya Michezo Jeshini na Jeshi limekuwa na Mchango mkubwa katika kuendeleza Michezo hapa nchini katika nyanja zote ikiwemo katika Ngumi.” Alisema Beatrice.
Aliongeza kuwa mbali na Mgeni rasmi lakini kwa Upande wa Maandalizi yote yamekalika na tunataraji kupata watu wengi wapenzi wa Ngumi ambao walikuwa wakishindwa kuhudhuria kutokana na mazingira ya kumbi lakini katika ukumbi huu usalama ni wa uhakika wa mashabiki na Mali zao.
“ Tumeandaa Pambano kwa Kuwashirikisha wa Ngumi za Wazi ili kutimiza Malengo ya Waaandaaji ambayo ni kuamsha hisia na Mashabiki wa Ngumi na kurejesha upinzani uliokuwa ukijitokeza wakati wa miaka ya Nyuma katika ngumi’ Alisema Beatrice.
Pia Aliongeza kuwa Anawashukuru kamisheni ya Ngumi za za Kulipwa nchini kutokanana kuidhinisha pambano na pia kutoa ushirikiano ikiwemo kuandaa waamuzi watakaohakikisha mchezo huo unafanyika kwa kufuata sheria zote za Mchezo huo.
Aidha alisema kama ilivyokuwa kwa Kamaisheni ya Ngumi za Kulipwa na Shirikisho la Ngumi za Wazi OBFT nako wamebariki kuchezwa kwa pamabno hilo kutokan na kushirikisha Wachezaji wa Ngumi za wazi wenye Upinzani wa Jadi Ngome na Jeshi la Kujenga Taifa JKT.
Miongozi mwa Wachezaji wanaotaraji kuonyesha mchezo mzuri katika Ngumi za Wazi ni Selemani Kidunda ambaye ni Nahodha kwa Ngome,Hafidh Mlawa wa JKT , Ismail Galiatano wa Ngome, Swahibu Ramadhani wa JKT Sambamba na Steven Anastaz wa JKT ambao wote wameitwa timu ya Taifa ya Ngumi..
Kwa upande wa ngumi za kulipwa Nasib Ramadhani atapambana na Bondia ambaye hajawahi kupigwa kwa KO Mohamed Kashinde wakati Baina Mazola na Kudura Tamimu kutoka Morogoro huku Bingwa wa Ngumi na Mateke Jeremia Joshua atacheza na Hashim Masungo wakati kaisi Ally atamenyana na Bakari Mohamed.