
Bondia Muingereza Anthony Joshua akiwa chini baada ya kuangushwa na mpinzani wake, Mmarekani mwenye asili ya Mexico, Andy Ruiz Jr Alfajiri ya leo ukumbi Madison Square Garden mjini New York kwenye pambano la uzito wa juu. Joshua amevuliwa ubingwa wa dunia wa uzito wa juu duniani baada ya kupigwa kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba. Ruiz hajawahi kuangushwa kabla, lakini naye leo alikalishwa chini raundi ya tatu, kabla ya kuinuka na kuendelea.
Sign in to your account
