NJOMBE
Aliyekuwa mchezaji na nahodha wa klabu ya Yanga na kupita katika vilabu mbalimbali vya soccer nchini kama kocha Shedraki Nsajigwa amewataka vijana kutoka wilaya nne za mkoa wa Njombe kushiriki katika ligi ya Kitulo drinking Water Cup itakayohusisha vilabu bora kutoka wilaya zote za mkoa huo ili kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wao na kusajiliwa na timu kubwa nchini.
Nsajingwa ambaye ndiye msimamizi wa mashindano hayo ametoa rai hiyo mjini njombe wakati akitangaza kuanzishwa kwa ligi hiyo ambayo itahusisha vilabu zaidi ya arobaini kwa lengo la kutoa nafasi kwa vijana kucheza mpira ambao umekuwa ajira ya uhakika katika dunia ya sasa .
Akitaja aina ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi mchezaji huyo wa zamani wa Yanga amesema kutakuwa na zawadi ya fedha taslimu Laki 5 kwa bingwa huku nyingine zikiwa ni zawadi ya msindi wa pili atakaepata laki 3 ,watatu akipata laki 1 huku nyingine akizitaja kuwa zawadi ya timu yenye nizamu,mfungaji boramwandishi bora na mtangazaji bora.
Nae Pilly Nyenje maarufu mama nyeupe ambaye ni barozi na Jeremia Chabata meneja wa kampuni iliyoandaa mashindano wanasema wamelazimika kufanya hivyo ili kurejesha kwa jamii na kutoa nafasi kwa vijana kuonyesha vipaji vyao.
Kuanzishwa kwa mashindano haya kumetafsiriwa kuwa kutaongeza ushindani katika msimu wa ligi ya mkoa ambayo itaanza kulindima mwezi mmoja mbele baada ya ligi hii kuisha , jambo ambalo linamfanya katibu wa chama cha mpira mkoa wa Njombe Njorefa VICENT MAJIRI kutoa kauli.
Kunywa maji tukutane uwanjani ndiyo kauli inayotumika katika michuano hiyo 2019.