Home Michezo Zawadi ya mshindi wa pili fainali za shirikisho

Zawadi ya mshindi wa pili fainali za shirikisho

0

Mshambuliaji wa Azam, Obey Chirwa akimtoka Mlinzi wa Lipuli N. Lufunga katika mechi ya fainali ya ubingwa wa mashindano ya Shirikisho la Azam iliyochezwa kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi Juni 1, 2019. Azam ilishinda 1-0. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Mshambuliaji wa Azam, Donald Ngoma akichanja mbuga kuelekea lango la Lipuli huku akizongwa na mlinzi wa Lipuli Haruna Shamte katika mechi ya fainali ya mashindano ya Shirkisho la Azam kwenye uwaja wa Ilulu mjini Lindi Juni 1, 2019. Azam ilioshinda 1-0. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkiuu)

****************************************

Klabu ya Lipuli fc imepokea kichapo cha goli 1:0 kutoka kwa wanalambalamba Azam fc ambapo mchezo huo ulikuwa fainali na Azam kutangazwa kuwa Mabingwa wa Michuano ya Kombe la Shirikisho.

Baada ya kwenda mapumziko kwa timu zote mbili Azam walikuja katika kipindi cha pili kuonesha kweli wanahitaji kombe hilo hivyo mpaka kufikia dakika ya 65 Obray Chirwa kufanikiwa kuingia kambani na kufanikisha timu yake kuchukua taji hilo

Katika matokeo hayo timu ya Lipuli FC ambayo ni mshindi wa pili imeibuka na kitita cha sh million 25.