NJOMBE
Waziri wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEM Selemani Jafo amefanya ukaguzi katika mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Palangawano na mradi wa hospitali ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe na kuonesha kuridhishwa mwenendo wa utekelezaji wa miradi hiyo ambayo amesema imezingatia vigezo vyote vilivyotolewa na serikali.
Wilaya ya Wanging’ombe ni wilaya changa zaidi mkoani Njombe ambayo imekuwa na changamoto kubwa zaidi ya huduma za afya hali ambayo imeisukuma serikali kufanya wa hospitali ya wilaya pamoja na ujenzi wa vituo vya afya vitatu na zahanati 2018/19 ili kumaliza changamoto hiyo ambayo imekuwa ikihatarisha maisha ya wagonjwa wengi wanaosafiri umbali mrefu kufata huduma hospitali ya rufaa na hospitali binafsi ikiwemo hospitali ya Ilembula.
Akizungumza na hadhara mara baada ya kukagua mradi wa kituo cha afya Palangawano na hospitali ya wilaya inayojengwa Ihanja Waziri Jafo amesema kufuatia changamoto kubwa ya huduma za afya wilayani humo serikali imeongeza mil 500 katika bil 1.5 iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya huku pia ikitoa zaidi ya mil 154 zahanati ya Isindagosi.
Nae mkurugenzi wa halmashauri hiyo Edes Lukowa, Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Comrade Ally Kassinge na Antony Mahwata wanaeleza jitihada walizochukua na changamoto walizokumbana nazo katika utekelezaji huku mvua ikitajwa kuwa kikwazo.
Kwa upande wao wakazi wa Ihanza na Palangawano wamezungumzia ujenzi wa kituo cha afya na hospitali ya wilaya utakavyonusuru maisha ya wagonjwa wengi huku wakidai awali walikuwa wakipata wakati mgumu kupata huduma.
Licha ya kuridhishwa na ujenzi lakini Jafo anatoa agizo ifikapo juni 30 kumaliza ujenzi hospitali zote za wilaya .