Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel wakimfanyia upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo kwenye paja mtoto mwenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo “Congenital Heart Disease” wakati wa kambi maalum ya matibabu ya siku saba inayofanywa na madaktari hao katika taasisi hiyo. Jumla ya watoto 11 wenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji mdogo wa moyo wa bila kufungua kifua na hali zao zinaendelea vizuri