Home Michezo Romario Sports 2010 limited kutengeneza jezi za Taifa Stars

Romario Sports 2010 limited kutengeneza jezi za Taifa Stars

0

*****************************************

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Romario Sports 2010 limited kwa ajili utengenezaji wa jezi za timu za Taifa.

Rais wa TFF Wallace Karia amesema kwamba kuanzia sasa wakati wowote shirikisho hilo litaanza kuwachukulia hatua watu wote ambao wanauza jezi feki.

Amesema kwamba mkataba huo una faida kubwa kwa TFF kwani kwa Sasa shirikisho hilo halitatumia gharama ya kununua jezi na pia watapa faida ya asilimia 15 kwa kila jezi itakayouzwa.