Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipewa zawadi ya fimbo mara baada ya kuvishwa vazi aina ya kikoi ikiwa ni ishara ya kumpongeza kwa utendaji kazi wake mzuri katika masuala ya Uhifadhi wa Wanyamapori wakati wa mkutano kati ya Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) na Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) kwenye mkutano wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa uhifadhi wa Wanyamapori nchini uliofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na nNyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa uhifadhi wa Wanyamapori nchini uliofanyika leo jijini Dodoma. SWengine ni watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wafanyakazi wa WWF.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya za Hufadhi za Wanyamapori George Wambura akizungumza na akizungumza na Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) kwenye mkutano wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa uhifadhi wa Wanyamapori nchini uliofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa mkutano wa Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs)
( Picha zote na Wizara ya Maliasili na Utalii)