Mwenyekiti wa baraza la elimu ya Ufundi NACTE John Kondoro, kulia akimuelekeza jambo Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha katikati, wakati akiwasili kabla ya kufungwa kwa maonyesho hayo leo, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Averina Semakafu.
Mhadhiri wa chuo cha College of Agriculture and Natural Resources, Deodatus Tibenda akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha, juu ya shughuri zinazofanywa na chuo hicho kabla ya kufungwa kwa maadhimisho hayo leo Jijini Dodoma.
Baadhi ya wawakilishi wa Taasisi mbalimbali wakiwa katika hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Elimu ya Ufundi NACTE Adolph Rutayuga akizungumza wakati wa hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi NACTE, John Kandoro, akizungumza wakati wa hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi a Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha, akizungumza wakati wa hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, akiwapungia mikono wadau wa maonyesho ya Elimu ya Ufundi, wakati wa hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wadau na wamiliki wa taasisi zilizoshiriki katika maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha, amesema elimu ya ufundi ni muhimu katika maendeleo, kwa sababu inakuza taaluma hasa kipindi hiki cha kutengeneza uchumi wa Viwanda.
Naibu Waziri Ole Nasha ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akifunga maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yaliyofanyika uwanja wa Jamhuri Dodoma yenye lengo la kukutanisha taasisi zote zilizochini ya NACTE.
Amesema kama Elimu ya Ufundi itasimamiwa kikamilifu italeta tija hasa kipindi hiki tunajenga uchumi wa viwanda, kwa sababu elimu ya ufundi inasaidia kukuza wataalamu ambao watasaidia katika viwanda.
Aidha amefurahishwa katika maonyesho hayo kuona vijana ambao ni mazao ya vyuo vya ufundi wakiwa na bidhaa mbalimbali ambazo wamezitengeneza wenyewe na kujiajiri kupitia elimu ya ufundi.
“Ndugu zangu nimepita kwenye mabanda humo nimeona vijana ambao wametoka katika vyuo hivi na wamejiajiri na wanafanya kazi nzuri sana, hii elimu ya ufundi ni muhimu sana inazalisha wataalumu ambao watatusaidia katika viwanda na Nyanja mbalimbali tunapojenga uchumi wa viwanda” amesema Ole Nasha.
Aidha amesema serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wa sekta binafsi ambao wanamalengo ya kuleta mabadiliko kwa nchi hasa kipindi hiki cha ujenzi wa viwanda serikili itakuwa bega kwa bega kuwaunga mkono kuhakikisha sekta hizo zinasongambele.
Amesema serikali inathamini sana uwekezaji wa sekta binafsi kwa sababu zinamchango mkubwa sana na hasa katika kuinua elimu katika Nyanja mbalimbali hapa nchini.
“Ukiangalia hapa nchini kuna vyuo vya ufundi mia tano arobaini(540) na vyuo binafsi ni mia tatu kumi na tisa(319) vyote hivi ni vyuo vya watu binafsi vya serikali ni kama mia mbili tu na kidogo, unaona sasa sekta binafsi ilivyo na mchango mkubwa” amesema Ole Nasha.
Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa baraza la Elimu ya Ufundi nchini NACTE Adolph Rutayuga, amesema maonyesho hayo yalikuwa na mafanikio makubwa, na wamedhamilia kuyafanya kuwa endelevu na baraza litaendelea kuyaboresha ili kuwa bora zaidi.
Amesema lengo la maadhimisho hayo ni kukuza taasisi hizo na kubadilishana uzoefu miongoni mwa taasisi hizo, na ni fulsa kwa wanafunzi wa taasisi hizo kujiajiri na kubainisha kuwa miongoni mwa waliokuwa wakitoa maelezo katika mabanda hayo ni wanafunzi wa taasisi hizo.
“Mheshimiwa maadhimisho hayo yamekuwa ya mafanikio sana na ili kuboresha zaidi kutekubaliana yawe ya kila mwaka angalau mara moja kuzikutanisha taasisi hizi kukutana kwa pamoja,na tumedhamilia katika maadhimisho yajayo kuongeza taasisi nyingi zaidi katika maonyesho haya” amesema Rutayuga.
Maadhimisho haya yalianza tarehe 27 mwezi huu nayamefungwa rasmi leo ambapo yamedumu kwa siku tano yaliyokuwa na lengo la kukutanisha taasisi zote zilizopo chini ya NACTE ili kuzitangaza taasisi hizo na maonyesho yalibebwa na kauli mbiu isemayo, “Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda Tanzania”.