Mwanasheria wa NEMC,Wakili Manchare Heche akiwasilisha mada katika Semina kwa waandishi wa habari juu ya katazo la mifuko ya plastiki hapo jana katika ukumbi wa mkutano wa NEMC jijini Dar es Salaam.
Dkt. Madoshi Makene akidadavua jambo katika Semina kwa waandishi wa habari juu ya katazo la mifuko ya plastiki
******************************************
Baadhi ya viwanda vimejitokeza ambavyo vinazalisha madawati pamoja na mabomba kutokana na malighafi yatokanayo na mifuko ya plastiki na kusaidia kuunga mkono juhudi za serikali kutokomeza taka hizo ambazo ni hatarishi kwa wanyama na samaki.
Moja ya viwanda ambavyo vitafanya zoezi hilo ni pamoja na kiwanda cha Falcon kilichopo Mwanza.
Ameyasema hayo leo , Waziri wa Muungano na Mazingira Mh. January Makamba katika utoaji elimu kwa wanahabari juu ya zoezi la ukatazaji wa matumizi ya mifuko ya plastiki.
“Tayari hivyo viwanda vinazalisha hizo bidhaa, mabomba na madawati na vinafanya hivyo kwa kuagiza malighafi nje ya nchi kama mchelemchele wa plastiki kwahiyo kwa kipindi hiki hata huo mchelemchele hutengenezwa kutokana na bidhaa za plastiki, kwahiyo badala ya kuangiza malighafi kutoka nje kwa kipindi hiki wanatengeneza mchelemchele humuhumu kwa bidhaa hizo, kwahiyo zitakapoisha wataendelea kuagiza marighafi kutoka nje”.
Waziri huyo ameongeza kuwa kuondoa taka zote za plastiki kwa wakati mmoja inakuwa ni ngumu kwasababu kuna bidhaa ambazo zinaulazimu zifungwe na mifuko hiyo ambayo wameamua kuziruhusu kufanyika kwa matumizi.
Kwa upande wa Mwanasheria NEMC Wakili Manchare Heche amesema kuwa bila kuathiri masharti ya kanuni ya 5, ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza vinywaji au bidhaa nyingine zikiwa zimefungashwa kwenye vifungashio vya plastiki isipokuwa tu kama aina ya bidhaa hizo inalazimu kutumia vifungashio vya plastiki.
“Kitendo cha kumiliki au kutumia mifuko ya plastiki , adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi 30,000/= lakini isiyozidi shilingi laki mbili au kifungo kisichozidi siku saba au vyote kwa pamoja”. Amesema Bw. Heche.
Mwongozo kwa wakaguzi na watekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki kwa halmashauri zote ni kwamba watakaokaidi au kutotoa ushirikiano katika ukaguzi au kuzuia au kuhujumu utekelezaji wa sharia au kuendelea kufanya makosa baada ya kuelekezwa au kupewa adhabu , watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali Zaidi kwa mujibu wa sharia za nchi.