Home Mchanganyiko KWANDIKWA AITAKA TBA KUKAMILISHA UJENZI WA JENGO LA NEC DODOMA

KWANDIKWA AITAKA TBA KUKAMILISHA UJENZI WA JENGO LA NEC DODOMA

0

NAIBU  Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa akielekea katika ukaguzi wa Majengo ya ofisi za Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) inayojengwa  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) iliyopo eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Kaimu Mkurungezi wa idara ya ujenzi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Humphrey Killo, kulia akitoa maelezo kwa Naibu  Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Majengo ya ofisi za Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC)  iliyopo eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Naibu  Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa akiwa katika ukaguzi wa  ujenzi wa Majengo ya ofisi za Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC)  iliyopo eneo la Njedengwa jijini Dodoma kulia kwake ni Kaimu Mkurungezi wa idara ya ujenzi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Humphrey Killo.

Moja ya jengo la ofisi za Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) linalojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) lililopo eneo la Njedengwa jijini Dodoma

Naibu  Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wanaosimamia ujenzi wa  Majengo ya ofisi za Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC)  yaliyopo eneo la Njedengwa jijini Dodoma kulia kwake ni Kaimu Mkurungezi wa idara ya ujenzi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Humphrey Killo.

Naibu  Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua wa  ujenzi wa Majengo ya ofisi za Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC)  iliyopo eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

  Kaimu Mkurungezi wa idara ya ujenzi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Humphrey Killo,akizungumza na waandishi wa habari.

Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

NAIBU Waziri  wa Ujenzi Elias Kwandikwa amewataka Wakala wa Majengo Tanzania  (TBA) kukamilisha ujenzi wa jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) kwa muda waliopewa ili lianze kutumika mapema kabla ya uchaguazi kuanza.

Mhe.Kwandikwa aliyasema hayo  jana jijini Dodoma wakati alipofanya ziara ya kukagua  mradi huo wa ujenzi wa jengo la NEC lililopo eneo la  Njedengwa UDOM.

“Mwakani kutakuwa na uchaguazi hivyoujenzi unatakiwa kukamilika kwa muda unaotakiwa ,lakini pia nimeambiwa kuna jengo ambalo litakamilika ndani ya mwezi mmoja na tume wataanza kufanyia kazi hapo”amesema Kwandikwa

Alisema lengo la Serikali ni kuwa tume hiyo iweze kuyatumia majengo hayo kwenye kutangaza matokeo ya  uchaguzi  mkuu ujao  pamoja na uchaguzi wa Serikali za mitaa zinazotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Hata hivyo alishauri kama kuna changamoto zilizopo kati ya mtekelezaji wa ujenzi wa mradi huo ambao ni Tba wakae na Tume ili kasi ya ujenzi hiyi iongezeke

Kwa upande wake Kaimu mkurungezi wa idara ya ujenzi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Humphrey Killo alisema ujenzi wa majengo hayo unatarajiwa kukamilika octoba mwaka huu na utagharimu zaidi ya sh bilioni 13 .

Bw.Killo ametoa rai kuwa wataendelea kushirikiana kwa pamoja nayale malengo tuliyojiwekea kwa pamoja tutafikia kwa msaada wa wizarana timu yetu nzima ya TBA.

“Tunatarajia mradi huu kama hakutakuwa na mkwamo wa fedha tukamilishe kazi zilizobaki kufikia Octoba 7 mwaka huu ndio mpango wetu wakazi upo hivyo kama hakuta kuwa na mkwamo wa fedha ambao haturajii utokee  ili angalau tume iweze kuemndelea na mipango yake kama ilivyokuwa imejipangia”amesema