**********************************************
Na Ahmed Mahmoud Karatu
Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo amegoma Kupokea Nyumba ya walimu ambayo inadaiwa kugharimu shilingi Milioni 52, zikiwa ni fedha kutoka kwa wafadhili milioni 34, nyingine zikitolewa na wananchi pamoja na serikali.Katika mradi huo, Wananchi wameoa kiasi cha milioni Tisa, huku serikali ikitoa pia milioni Tisa kwaajili ya upauzi wa jengo.Kwa upande wao wafadhili wa mradi huo wamekiri uwepo wa mapungufu hayo na kuahidi kuyafanyia Kazi.Kuhusu msaada wa ujenzi wa Bweni la Wasichana pamoja na Bwalo la Chakula, Mkuu wa wilaya Mahongo amepongeza ujenzi huo, huku Meneja wa African Foundation, Mkomeni Ernest, amasema lengo ni kuhakikisha jamii inanufaika na uwepo wa makampuni yanayozunguka hifadhi zilizo karibu na wananchi.