Afisa Mazingira wa Jiji la Dodoma Ally Mfinanga akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wa Jamhuri Sekondari baada ya zoezi la ukusanyaji wa mifuko ya plastiki katika eneo linalizunguka Shule hiyo.
Diwani wa Kata ya Uhuru Jijini Dodoma, Ally Kheri akizungumza baada ya tamati ya zoezi la ukusanyaji mifuko ya plastiki kuzunguka shule ya sekondari Jamhuri zoezi lililoshirikisha ofisi ya afisa mazingira na kampuni ya usafi ya Green West.
Meneja wa kampuni ya usafi ya Green West Abdallah Mbena akizungumza baada ya tamati ya zoezi la ukusanyaji mifuko ya plastiki kuzunguka shule ya sekondari Jamhuri.
Afisa mazingira wa kata ya Uhuru akizungumza baada ya tamati ya zoezi la ukusanyaji mifuko ya plastiki kuzunguka shule ya sekondari Jamhuri zoezi lililoshirikisha ofisi ya afisa mazingira na kampuni ya usafi ya Green West.
Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Jamhuri Neema Leonard akizungumza baada ya tamati ya zoezi la ukusanyaji mifuko ya plastiki kuzunguka shule ya sekondari Jamhuri zoezi lililoshirikisha ofisi ya afisa mazingira na kampuni ya usafi ya Green West.
Wafanya kazi wa kampuni ya usafi ya Green West pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Jamhuri na baadhi ya viongozi wakifanya usafi wa kuondoa mifuko kwa kutekeleza katazo la Serikali kwa Mifuko ya Plastiki.
Sehemu ya picha ya pamoja baada ya kumaliza kufanya usafi kwa kukusanya mifuko.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
…………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Jiji la Dodoma katika kuunga mkono agizo la serikali la kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki ili kulinda mazingira, limeanzisha mfumo wa kuwahamasisha wananchi kuondoa mifuko hiyo katika mazingira yao, na kutoa elimu kuachana kabisa na matumizi ya mifuko hiyo na kutumia mifuko mbadala.
Akizungumza wakati wa zoezi la hamasa ilikuhamasisha wanachi kuondoa mifuko ya plastiki katika maeneo yao afisa mazingira wa Jiji la Dodoma Ally Mfinanga, amesema wao kama jiji wanaonyesha kwa vitendo kuitikia agizo hilo kwa kuwahamasisha wananchi kuondoa mifuko hiyo ili kuacha mazingira yakiwa safi.
Sambamba na hilo amesema wanawaelimisha wananchi kuacha na matumizi ya mifuko ya plastiki na kutumia mifuko mbadala ili kuweka mazingira safi.
“ Tumeitikia kwa vitendo agizo la Waziri mkuu la kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki, na sisi kama unavyoona leo hii tupo shule ya sekondari jamhuri hapa, ni katika kutoa hamasa kwa wananchi kuacha na matumizi ya mifuko ya Rambo ambayo inamadhara makubwa katika ustwi wa mazingira”,
“Amesema wao kama jiji wanajitahidi kuwafikia wananchi katika na kuwapa elimu ili watumie mifuko mbadala tulinde mazingira yetu yawe na safi na sisi tuwe mfano kwa kuwa jiji safi” amesema mfinanga.
Amesema endapo wananchi wote kwa pamoja wakikubaliana kwa kauli moja kuachana matumizi ya mifuko ya plastiki basi adhima ya serikali itafikiwa, amewakumbusha wanachi kuondoa mifuko popote ilipo na atakaye kutwa anatumia mifuko hiyo faini ni shilingi elfu therathini(30000).
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Uhuru, Ally Kheri ameshukuru wananchi kwa kujitikeza kwa wingi katika zoezi hilo na kusema baada ya kusikia kampeni hiyo walikaa na kamati ya ODC na kukubaliana kuanza na taasisi zilizopo katika kata hiyo.
Walianza na Shule ya Uhuru kasha wakafuatia na sekondari ya Central na leo wamefika katika shule ya Sekondari Jamhuri na kupata mwitikio mkubwa na zoezi kufanyika kwa mafanikio mmakubwa sana.
“Kwanza nishukru kwa kufanikiwa kwa zoezi hili na wanachi wameitikia kwa kiwango kikubwa sisi kama kata baada ya kusikia kampeni hii tulikaa kamati ya ODC na tukakubaliana kuwa tuanze na maeneo ya taasisi tulianza na shule ya Uhuru, Sekondari Central na leo tupo hapa Jamhuri zoezi limefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana”
Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya usafi ya Green West Abdallah Mbena ameishukuru serikali kwa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kwani ilikuwa ikiletaufumbufu katika kuweka mji safi lakini kwa sasa kazi yao itarahisishwa kwa kiwango kikubwa.