Waandishi wa habari wakimsikiliza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb). |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa 109 wa Baraza la Mawaziri wa nchi za Afrika, Karibiani, na Pasifiki (ACP) uliofanyika Brussels, Ubelgiji kuanzia tarahe 20 hadi 22 Mei 2019. Mkutano huu, ulifuatiwa na Mkutano wa 44 wa pamoja wa Mawaziri wa nchi za ACP na wenzetu wa Umoja wa Ulaya (EU) ambao ulifanyika mnamo tarehe 23 na 24 Mei 2019.
Akizungumza hivi karibuni Dkt. Ndumbaro amesema Katika mkutano huu,upande wa Tanzania aliongozana na Watendaji Waandamizi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Fedha na Mipango, na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pia, Watalaam kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Brussels, walishiriki mikutano hiyo.
Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema katika mikutano yote miwili, majadiliano yalijikita katika maeneo makuu matatu. Mosi, ni kupitia na kutathimini utekelezaji wa makubaliano na mipango mbalimbalin walionayo ndani ya nchi za ACP na baina ya nchi za ACP na EU. Pili, kuainisha, kujadili, na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika ushirikiano ndani ya nchi za ACP na baina ya nchi za ACP na EU. Tatu, kutoa muongozo juu ya mustakabali wa ushirikiano tunaotarajia uwepo ndani ya nchi za ACP na baina ya nchi za ACP na EU katika kipindi kijacho.
“Kwa upande wa agenda ya kwanza, tulipitia utekelezaji wa makubaliano ya programu mbalimbali ndani ya nchi za ACP na baina ya nchi za ACP na EU. Programu hizo ni pamoja na zile zinazohusu masuala ya ubia wa kimaendeleo, biashara, masoko, kilimo, elimu, maendeleo ya sekta binafsi, teknolojia, mifumo ya kodi, uhifadhi wa mazingira, hifadhi ya bahari, na masuala mengine yanayofanana na hayo. Kwa ujumla tulikubaliana kuwa programu hizi ni muhimu katika kuchochea kasi ya maendeleo ya nchi zetu na zikaendelea kutekelezwa kwa kasi inayostahili, mgawanyo ulio sawa na kwa kuzingatia mahitaji ya nchi husika”.
“Kwa mfano, katika eneo la kilimo, Tanzania ilitoa hoja ambayo baada ya majadiliano ya kina ilikubalika kuongeza mazao ya korosho, pamba, na kahawa katika orodha ya mazao yaliyopo katika mpango wa mwaka 2019 wa utekelezaji wa programu ya ACP ya kuendeleza mnyororo wa thamani katika mazao ya kilimo”.
Hata hivyo Dkt. Ameongeza kuwa Mpango huu unafadhiliwa na EU na umetengewa kiasi cha Euro milioni 125. Katika zao la korosho, nchi wanachama wa ACP iliisifu na kuipongeza Tanzania kwa uamuzi wa kishujaa uliochukuliwa na Serikali chini ya uongozi thabiti wa Mhe.Rais Magufuli kwa kuzuia mwendelezo wa mdororo wa bei ya korosho na hatua za makusudi zinazoendelea katika kuongeza mnyororo wa thamani wa zao hilo.
Wakati wa mkutano huu, ujumbe wa Tanzania ulieleza kwa kina hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kujenga uchumi wa viwanda kwa lengo la kufikia uchumi wa kati. Miongoni mwa hatua tulizozieleza ni pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), mradi wa uzalishaji wa umeme wa mto Rufiji, ununuzi wa ndege na kufufuliwa kwa ATCL, ujenzi wa barabara, kupanuliwa kwa bandari, viwanja vya ndege na miradi mingine.
“Tulitumia nafasi hiyo kuzihakikishia nchi za ACP na Umoja wa Ulaya juu ya uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji na biashara nchini Tanzania na kuwajulisha kuwa Serikali kupitia mwongozo wa BLUEPRINT inatekeleza mikakati ya kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji na biashara”. Amesema Dkt. Ndumbaro.
Vilevile Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa Katika agenda ya kujadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika ushirikiano wetu, walibainisha na kujadiliana na wenzao wa Umoja wa Ulaya juu ya changamoto hizo na umuhimu wa kupata ufumbuzi wake.
“Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kasi ndogo ya utekelezaji wa baadhi ya programu za maendeleo, kiwango kidogo cha biashara baina ya nchi za ACP, kuendelea kuibuka kwa vikwazo vipya vya biashara visivyo vya kiforodha kwa bidhaa za ACP katika soko la Ulaya, sintofahamu inayoendelea baina ya nchi za ACP na Umoja wa Ulaya katika kusainiwa na kutekelezwa kwa Mikataba ya Ubia wa Kiuchumi (Economic Partnership Agreements – EPAs), na kuwepo kwa vikwazo kwa baadhi ya nchi wanachamaa wa ACP na kuwepo kwa maamuzi 4 yasiyozingatia misingi ya uhuru wa nchi (sovereignty), usawa (equal partnership), na kuheshimiana. Nchi za ACP, ikiwemo Tanzania, zilisisitiza changamoto hizi zipatiwe ufumbuzi haraka kwa kila upande unaohusika na tulikubaliana kuwa katika ushirikiano wetu ni muhimu kila upande ukaheshimu kanuni za ushirikiano, sheria na tamaduni za nchi husika”. Ameongeza Dkt. Ndumbaro.
Pamoja na hayo Dkt. Ndumbaro amesema Tanzania ikiungwa mkono na nchi nyingine za ACP haja na umuhimu wa kuzingatia na kuheshimu matakwa ya Ibara ya 12 ya mkataba wa ubia wa sasa unaojulikana kama Cotonou Partnership Agreement.Ibara hiyo inazuia upande wowote kuchukua uamuzi wenye madhara kwa upande mwingine bila kuingia kwenye mashauriano ya kina na
upande huo.
upande huo.