Wabunge wa viti maalum Mkoa wa Dar es salaam wamewataka wanawake wa umoja wa wanawake CCM (UWT) kuwa na umoja na mshikamano kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ili chama cha Mapinduzi kiweze Kupata ushindi wa kishindo.
Wabunge hao wametoa wito huowakati wa ziara yao mkoani Dar es salaam kutembelea wanachama wa UWT, ambapo wamesema iwapo wanachama hao watashirikiana ,kuacha makundi na kukisaidia chama, kitafanya vizuri katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge kazi na wenyeulemavu Mhe. Stella Ikupa , akizunguza katika ziara hiyo,amewashukuru wanawake wa umoja huo kwa kuendelea kuwaungamkono wabunge wanawake viti Maalumu mkoa wa Dar es salaam na kuwa taka kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa Kufanyika mwakahuu.
Aidha ameitaka UWT kuwahamasisha walevu kugombea nafasi katika uchaguzi huo na kuwaunga mkono kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi hakina ubauguzi.
“Nawashukuru sana kwa kuniamini katika uwakilishi nami nawakilisha walemavu wote nchini wakiwemo wa mkoa wa Dar es salaam,nilipo ingia Bungeni swali langu la kwanza lilikuwa kuhusu kupatiwa mikopo walemavu , nashukuru serikali ili kubali na sasa walemavu wanapatiwa asilimia mbili ya mikopo ya halmashauri ” Alisema Ikupa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angella Kairuki, alisema katika kujiandaa na uchaguzi Tathimini inatakiwa Kufanyika na kikubwa zaidi kufanyika maandalizi ya kutosha na kusema kuwa wasaliti wasipewe nafasi, pia kuwatia moyo wanawake kugombea nafasi ili kufikia uwianno wa 50kwa 50 katika uwakilishi .
“Tuna shukuru sana kwa kuwa mmeendelea kumpongeza Rais Magufuli na kumuunga mkono katika shuguli zake za kuleta maendeleo ya nchi endeleeni na moyohuo” Alisema Kairuki.
Katika kujikwamua kiuchumi Kairuki aliwataka wanawake hao kuchangamkia fursa za mikopo ya Halmashauri inayotolewa bila riba iweweze kujiendeleza kibiashara.
Kwaupande wake Mbunge wa viti Maalumu mkoa wa Dar es salaam,Mhe.Mariam Kisangi pamoja na kuwashukuru aliwataka akinamama hao kwenda kuhamasisha wanawake kujiunga na chama cha Mapinduzi nakuhamasisha wanawake kuchukua nafasi za kugombea .
‘’Niwajibu wetu kama wabunge kuwaelezea wanawake wenzetu waliotuchagua mambo makubwa ya maendeleo abayo serikali imeyafanya katika Wilaya zetu , majimbo na mkoa wetu kwa ujumla ,kunaujenzi wa daraja jipya la Salenda, Mradi wa DMDP umeboresha na kujenga barabara, ujenzi wa barabara ya Morogoro eneo la kimara,na mambo mengine ya maendeleo ambayo serikali yetu ya Chama Cha Mapinduzi inaendelea kuyafanya’’Alisema Kisangi.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa wanawake CCM (UWT) Mkoa wa Dar es salaam ,Grace Chrispine Haule , aliwapongeza madiwani wa kwa uchapa kazi na utiifu kwa umoja huo pamoja na wabunge wanawake wa mkoa wa Dar es salaam pamoja na kuwa na majukumu mengi ya Kitaifa lakini wamekiheshimu chama na wamekuwa wakiitika wito kwa umoja huo.
“Kwa sasa tuna nafasi chache za madiwani wa viti Maalumu naomba tujitahidi tupate ushindi ilituongeze viti sasa tunachofanya ni kuwafanya wanawake waweze kujiamini na tupate watakao gombea” Alisema
Pamoja na hayo Haule, amempongeza Rais Dr John Pombe magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya akishirikiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri mkuu Majaliwa, kwa kiasi kikubwa wametimiza ahadi walizo ahidi na anaamini katika uchaguzi ujao CCM itaendelea kushinda kwa kishindo.
Nao baadhi ya wanachama wa umoja huo wa mewataka wabunge hao kushughulikia kero za miundombinu ambayo imeharabika katika kipndi hiki cha mvu pamoja na Umeme na maji kwa ni kunamaeneo yanamahitaji huduma hizo.