Viongozi wastaafu walioweza kuhudhulia mkutano huo ambao ulikuwa unalenga kuzungumzia uzalendo uliopo barani Afrika kwa ujumla.
Mabalozi wa nchi mbalimbali wakiwa na viongozi wastaafu wakipata picha ya pamoja na Waziri wa Habari,Sanaa, Tamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika Ukumbi wa Nkurumal uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
*****************************************
Vijana watakiwa kutumia ujana wao kuweza kutetea uhuru wa nchi yao ili baadae waweze kuweka historia kwa mambo ambayo watakuwa wameyafanya.
Ameyasema hayo Waziri wa Habari,Sanaa, Tamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika tafakuri iliyoandaliwa na Uhuru Media katika Ukumbi wa Nkuruma Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema wakati tunapata uhuru miaka ya tisini wakoloni waliondoka nchini kimkakati wakiwa wameacha mfumo uleule na kuendeleza kuchukua madini yetu kwa bei ya chini na walichokifanya ni kulazimisha nchi za kiafrika kuingia mikataba ya kuendeleza misingi ileile ambayo muingereza au wafarasa waliiacha.
“Baba wa Taifa (Mwalimu Nyerere) alikuwa kiongozi wa kwanza barani Afrika aliyekataa kusaini mikataba endelevu ya waingereza, alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania wanakuwa wazarendo kutetea nchi yao”. Amesema Dkt. Mwakyembe.
Aidha Waziri huyo amewashukuru viongozi wa bara la Afrika kwa kukubali mwaka 2011 kuwa na programu ya urithi wa Ukombozi wa bara la Afrika ambayo lengo kubwa ni kuhakikisha hii leo sirikali zetu zinakusanya kwa pamoja nyaraka mbalimbali na kuhifadhi ushahidi wowote ule wa ukombozi wa bara la Afrika.
Kwa upande wake aliyekuwa Rais wa kwanza wa bunge la Afrika Bi.Getruda Mongera amesema kuwa nchi zetu zimekuwa tegemezi kwasababu wanaume tuliowakabidhi kuongoza nchi zetu wametuangusha. Tulipambana kuondoa Utumwa, Ukoloni na tumeshiriki pamoja katika mapambano ya kusini mwa Afrika pamoja nao, wametuangusha.
“Vijana msirudie makosa ya baba zenu hilo ni kosa, tusimnyooshee mtu vidole wakati huu wa sasa, tuachane na maneno ya ukosoaji”. Amesema Bi. Getruda.
Hata hivyo kwa upande wa Mhadhiri wa zamani wa chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Balozi Christopher Lihundi amesema kuwa elimu ya uzalendo ambayo tunahitaji tunaweza kuipata nyumbani, shuleni pamoja na ulimwenguni. Pamoja na kuamini, kulelewa na kuwekewa mazingira mazuri ya malezi kwasababu malezi bora yanaanza nyumbani.
“Uzalendo unamiiko yake, kwamba mtu mzarendo ni mstaharabu na awezi kufanya mambo ambayo wenzake wanachukia lakini wengine wanapoambiwa sio mstaharabu maana ustaharabu kauponyoka, hawaheshimu watu,vitu na hata rasilimaliza jumla haziheshimu”. Amesema Mh.Lihundi.