Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Digitali, Mifumo na Bidhaa kutoka NMB Benki, Ndg. Pete Novert walipokutana leo katika Shule ya Sekondari Mnyakongo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Katikati ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Ndg. Margaret Ikongo na Meneja wa NMB Benki Kanda ya Kati, Ndg. Nsolo Mlozi
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Ndg. Margaret Ikongo (katikati) na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Digitali, Mifumo na Bidhaa kutoka NMB Benki, Ndg. Pete Novert walipokutana leo katika Shule ya Sekondari Mnyakongo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnyakongo alipowatembelea leo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Meneja wa NMB kanda ya kati Nsolo Mlozi,akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnyakongo baada ya kwenda kukabidhi Viti,Meza na Mabati wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Shule ya Mnyakonga Mpokeeni Sanga,akitoa taarifa ya shule yake baada ya kupokea Viti,Meza kutoka benki ya NMB wilayani Kongwa Mkoani Dodpoma.
Diwani wa Kata ya Kongwa Mhe.White Zuber akitoa neno la shukrani kutoka kwa benki ya NMB mara baada ya kukabidhi Viti,Meza kwa shule ya Sekondari Mnyakongo pamoja mabati 250 kwa shule ya Chiwe zote za wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma
Mjumbe bodi ya wakurugenzi Benki ya NMB Margaret Ikongo akitoa semina kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari Mnyakongo na Chiwe baada ya kufanya ziara ya kukabidhi Viti,Meza na Mabati wilayani Kongwa Mkoani Dodoma
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnyakongo wamsikiliza Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai (hayupo kwenye picha) akizungumza baada ya kuitembelea Shule hiyo leo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai akikata utepe baada ya kukabidhiwa viti na meza kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mnyakongo zilizotolewa na Benki ya NMB tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mnyakongo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Kuanzia Kushoto ni Meneja wa NMB Benki tawi la Kongwa, Ndg. Tuntufye Mwakatika, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Ndg. White Zuberi, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Ndg. Margaret Ikongo, Afisa Mkuu wa Kitengo cha Digitali, Mifumo na Bidhaa kutoka NMB Benki, Ndg. Pete Novert na Meneja wa NMB Benki Kanda ya Kati, Ndg. Nsolo Mlozi
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai akikata utepe baada ya kukabidhiwa Mabati kwa ajili ya Shule ya Sekondari Chiwe yaliyotolewa na Benki ya NMB tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mnyakongo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Ndg. Margaret Ikongo
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimshukuru Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Ndg. Margaret Ikongo baada ya kukabidhiwa Mabati kwa ajili ya Shule ya Sekondari Chiwe yaliyotolewa na Benki hiyo tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mnyakongo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Picha na Alex Sonna
………………………
Na.Alex Sonna,Kongwa
SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameiomba Benki ya NMB kutoa elimu kwa wananchi ili wajue jinsi ya kutunza fedha za mikopo yao.
Ndugai ameyasema hayo wakati wa NMB ilipofanya ziara ya kukabidhi viti na meza 63 vyote vikiwa na idadi hiyo kwa Shule ya Mnyakongo pamoja na mabati 250 kwa Shule ya Chiwe zilizopo Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika amesema kuwa NMB wanakila sababu ya kutoa elimu ya utunzaji fedha kwa wananchi kama wanavyofanya kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ili wawe na ujuzi zaidi.
Aidha amesema kuwa watu wengi wanakopa fedha lakini hawajui wafanyie nini baada ya kuzichukua.
‘’Yaani unashangaa muda mchache ukikutana na watu hao hakuna cha maana walichofanyia badala yake wanarudi katika maisha ya chini badala ya kusonga mbele kimaisha’’amesema Ndugai
Spika Ndugai amesema kutokana na hilo kuna sababu ya elimu hiyo kutolewa kwa wananchi ili wakope fedha huku wakijua wanakwenda kuzifanyia nini.
Ndugai amefafanua kuwa ameshakutana na kesi hizo nyingi kwa ndugu jamaa na marafiki ambao wamekopa bila ya kupata mafanikio yoyote.
‘’Kwa kweli kwa hilo naomba mlifanyie kazi kwani limekuwa likiwaumiza wananchi na kupelekea kurudi nyumba kimaendeleo badala ya kwenda mbele katika maisha kupitia fedha walizokopa’’amesisitiza Ndugai
Kwa upande wake Meneja wa NMB kanda ya kati Nsolo Mlozi amesema kuwa wataendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli hivyo wametenga maeneo manne kwa ajili ya kusaidia jamii.
Mlozi ameyataja amaeneo hayo ni Elimu,Afya,Kilimo na utunzaji Fedha kwa vijana mpaka watu wa rika la juu kwa lengo la kuwainua kiuchumi kwa kunufaika kwa kupitia NMB.
Hata hivyo amesema kuwa mpaka sasa tayari milioni 400 zimeshatolewa kwa ajili ya misaada katika shule na hospitli ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa.Mlozi amesema kuwa NMB iko pamoja na serikali kuhakikisha wanafikia malengo waliojiwekea.
Naye Mkuu wa Shule ya Mnyakonga Mpokeeni Sanga amesema kuwa walikua na upungufu wa madawati 70 na wanaishukuru NMB kuwapa viti 63 na meza 63 na ambavyo wanaamini vitasaidia kupunguza uhaba waliokuwa nao.
Sanga amewahakikishia NMB kuwa vitu hivyo watavitunza ili hapo wanafunzi wengine waje kuvitumia hapo mbeleni na amewaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia jamii kwani wamekuwa mfano wa kuigwa nchini.
Mkuu wa shule ya Chiwe Aron Mango amesema kuwa mabati hayo waliopewa yatawasaidia kuezeka mabweni ya wasichana ambayo yanajengwa shuleni hapo