Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe Ibrahim Juma(katikati) akisajili  laini  ya simu kwa alama za vidole katika kampuni za simu ya Smile,kushoto  ni Mackie Mdachi  na Arnold Ntiga, ambao ni wasajili kutoka kampuni hiyo.Usajili huo umefanyika leo kwenye ukumbi  namba moja wa Mahakama ya Rufaa Tanzania..

Majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Mhe. Winfrida Korosso,(kulia), Mhe. Rehema Mkuye(katikati) na Mhe. Barke Mbaraka Sehel(kushoto) wakisikiliza maelezo kuhusu usajili laini za simu kwa vidole wakati  wakijisajili zao  leo katika kampuni ya simu ya Halotel. Usajili huo umefanyika leo kwenye ukumbi namba moja wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.           Dkt.Eliezer Feleshi akisajili laini  ya simu kwa alama za vidole katika Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kulia aliyevaa shati la kitenge  ni  Afisa Mauzo wa TTCL, Usajili huo umefanyika leo kwenye ukumbi namba moja  wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Mhe, Rehema Mkuye akisajili laini ya simu kwa alama za vidole  katika kampuni ya Halotel. Usajili huo umefanyika leo kwenye ukumbi  namba moja wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Mhe, Augustine Mwarija akisajili laini ya simu kwa alama za vidole  katika kampuni ya  Vodacom. Usajili huo umefanyika leo kwenye ukumbi namba moja  wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.Kushoto ni  anayemsajili ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Vodacom Happiness Shuma.

Baadhi ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakisajili laini za simu  kwa alama za vidole katika kampuni mbalimbali za simu, wakati wa usajili huo uliofanyika leo kwenye ukumbi namba moja  wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

(Picha na Magreth Kinabo.)