Zaidi ya Wamiliki wa Nyumba 25 Elfu Wametakiwa Kukitumia Kipindi Cha Kuanzia Sasa Hadi Juni 30 Mwaka Huu Kukamilisha Zoezi la Ulipaji Kodi ya Majengo Yao Kabla ya Mwaka Mpya wa Fedha Kuanza Hapo Julai Mosi vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa.
Sheria ya Usimamizi wa Kodi Kila Mmiliki wa Jengo Atakayekaidi Kulipa Kodi Anapaswa Kupigwa Faini Au Kushtakiwa Mahakamani
Shabani Musib ambaye meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Njombe amesema mwamko umekuwa mdogo katika kulipa kodi ya majengo ilinganishwa na miaka mingine na kuwataka wamiliki wa majengo kufanya hivyo katika muda uliopangwa.
Kusuasua kwa ulipaji kumetajwa kusababishwa na idadi ndogo ya rasilimali za kutolea huduma ikiwemo watalaamu na vitendea kazi hatua ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi wengi hatua ambayo imetendewa kazi na mamlaka hiyo ambapo imewapa mamlaka Watendaji wa Vijiji,na Mitaa kukusanya kodi hizo ili kupunguza foreni.
Kutokana na mfumo huo mpya mamlakaya mapato mkoani humo imelazimika kuwakutanisha watendaji wa vijiji na mitaa na kuwapa elimu ya ukusanyaji akiwemo Zakalia Mligo na Neema Mtama wanasema hatua hiyo itakuwa na faida kubwa kwa walipa kodi sababu imepunguza usumbufu