Mwenyekiti wa kigoda cha mwalimu nyerere Prof. Rwekeza Mukandala akisimikwa mbele ya viongozi wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Nkurumah UDSM.
********************
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala amesema wasomi wananafasi kubwa katika kushauri serikali kuhusu masuala mbalimbali ya kimaendeleo ili kuzidi kukuza uchumi wa nchi.
Akizungumza leo wakati wa Tamasha la kitaaluma la 11 la kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere Prof. Mukandala amesema kuwa lengo kuu la tamasha ni kuangalia nafasi ya dola katika soko hulia na sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya nchi.
Hata hivyo Prof. Mukandala ameongeza kuwa taasisi mbalimbali za sekta binafsi na wasomi wamepewa kipaumbele kwa kufanya tafiti ili kuchangia pato la taifa ili kuweza kukuza uchumi wa nchi.
“kama tukimnukuu mwalimu nyerere alisema ili taifa lisonge mbele linaitaji ushirikiano wa kina wa kimaendeleo pamoja na ushirikishwaji wa jamii nzima”. Amesema Prof. Mukandala.
Naye Mdau wa Masuala ya Sekta Binafsi na Uwezeshaji Bw. Ali Mafuruki amesema ni vyema serikali ikawapa kipaumbele wadau wa sekta binafsi ili uchumi uzidi kusonga mbele hasa ukizingatia serikali ya awamu hii ikiweka kipaumbele Zaidi suala la uchumi.
“Serikali yetu iendelee kushirikiana na wadau wa masuala ya uchumi ili kuiendeleza kukua na kufika mbali zaidi kama ilivyo kwa mataifa mengine”. Amesema Bw.Mafuruki.
Aidha Bw. Mafuruki ameongeza kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote umekuwa ukitegemea ushirikiano baina ya sekta mbalimbali.