****************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
BODI ya maji ya Bonde la Pangani,imeanza kutoa mafunzo kwa watumiaji wa maji wa mito mikubwa ya Themi, Kikuletwa na Naura mkoani Arusha,ili kuwawezesha kuelewa rasilimali za maji waweze kuwajibika kuilinda,kuitunza na kuisimamia.
Hayo yameelezwa leo na Afisa maendeleo ya Jamii wa bodi ya Pangani,Abraham Yesaya alipokuwa akitoa mada kwenye mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo na uelewa watumiaji wa maji ya mto Themi,jijini ,Arusha yaliyofanyika kwenye kumbi wa Chama cha Mapinduzi CCM,mkoa wa Arusha
Yesaya, amesema kwenye mafunzo hayo kwamba kulingana na mabadiliko ya sera ya maji ya mwaka 20202 inawataka wananchi wenyewe washirikishwe na ndio wawe wasimamizi wakuu wa rasilimali za maji ambapo kila Kijiji kitakuwa na Kamati yake.
Amesema kwenye mafunzo hayo wananchi wanaibua changamoto wanazokabiliana nazo wakati wa kuimarisha usimamizi wa maatumizi mabaya ya maji kwenye mito hiyo mikubwa .
Amesema Serikali imekuja na makakati huo wa kuto mafunzo kwa wananchi Vijijini ili waweze kuelewa sheria za maji , usimamizi wake na uboreshaji wa mazingira ya mito hiyo ili isikauke na kuchafuliwakutokana na matumizi mabaya.
Yesaya,amesema kuwa bodi hiyo imeshatoa mafunzo kwa watumiaji wengine wa maji wa mito mikubwa ya Nduruma na Kikuletwa ,wilayani Arumeru, mafunzo ambayo lengo lake ni kuwajengea uwezo watumiaji wa maji kwenye mito hiyo ambapo wataunda uongozi wa kusimamia raslimali hizo na serikali itatoa msaada wa kiutaalamu na vitendea kazi .
Yesaya,amesema Kupitia mafunzo hayo wawekezaji waliopo kandokando ya mito hiyo vikiwemo Viwanda Hotel na mashamba ya maua watashiriki kikamilifu katika utunzaji na uboreshaji wa mito na vyanzo vingine vya maji vilivyopo kwenye maeneo hayo na hivyo kusitisha utiririshaji wa maji ya Viwandani mitoni..
Kuhusu uchimbaji wa Visima vya maji ,ameshauri usifanywe holela kwa kuwa madhara yake ni makubwa na kutahadharisha kuwa kukitokea tetemeko la ardhi itakuwa ni hatari kwa makazi kutokana na utitiri wa Visima.