Home Mchanganyiko RAIS Dkt Magufuli Ameipatia Heshima kubwa Tanzania kwa kuwa na Paspoti yenye...

RAIS Dkt Magufuli Ameipatia Heshima kubwa Tanzania kwa kuwa na Paspoti yenye Ubora wa Kimataifa -Uhamiaji

0

Afisa  wa  idara ya  uhamiaji  mkoa wa Iringa Tunu Ng’ondya akionyesha hati  mbali mbali za  kusafiria nje ya Tanzania  jana wakati  alipozungumza na wanahabari  kuhusu  kujaza fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote(picha na Francis Godwin)

……………………….

Na Francis Godwin ,Iringa

Ofisa  uhamiaji mkoa wa Iringa  Tunu Ng’ondya amesema  amepongeza  jitihada mbali mbali  zinazoendelea  kufanywa na  serikali ya awamu ya tano  chini ya Rais Dkt  John  Magufuli  katika  kuboresha  idara   hiyo  na  kupelekea  kuliletea  Taifa   heshima kubwa  katika  dunia  kwa  kuwa na hati ya  kusafiria nje ya Tanzania   yenye ubora  wa  kimataifa .

Akizungumza na  waandishi wa habari jana ofisini kwake kuhusu  kujaza fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote   Ng’ondya  alisema   kuwa  kabla ya  jitihada  za  serikali ya awamu ya tano  kufanyika  pass hiyo ya  kusafiria ilikuwa  katika  hali ya  ubora  wa chini  ila  baada ya  kutoa  fedha  kwa  ajili ya  kuboresha  idara ya  uhamiaji  hivi sasa  kati ya hati bora  za  kusafiria  duniani  hati ya  Tanzania  ni  miongoni na  hivyo imeweza  kuingia katika ubora  wa  ulimwengu .

Hata  hivyo aliwataka  wananchi kufika  katika  ofisi za  uhamiaji  kukata  pass za  kusafiri ili  kuweza  kuchangamkia fursa  mbali mbali  za  kibiashara  nje ya Tanzania  kwa  kwenda  kufuata bidhaa na  kuja  kuuza  nchini ama  kupeleka  bidhaa zinazozalishwa na  watanzania  kuuza  nje ya Tanzania.

Alisema serikali  imeweka utaratibu  mzuri  wa kila mwenye    sifa  ya  kuwa na hati ya  kusafiria  kuweza  kumiliki pasipo  usumbufu  wowote na  kuwa suala la maombi na malipo ya  gharama za kupata pass  hiyo yanafanyika  kwa  njia ya mtandao  na kuwa  ofisi  yake haipokei  fedha  yoyote  taslim kutoka kwa  mwombaji isipo kuwa mwombaji anapaswa  kufika ofisini akiwa na viambatanishi vya vinavyohitaji baada ya  kufanya maombi kupitia mtandao .

” Kama  kuna  mtu  ataombwa   fedha taslimu  na  ofisa  yeyote atakapofika ofisini kwangu naomba achukue  jina la  mhusika na  kuniletea  ili achukuliwe  hatua kali  za   kinidhamu kwani hatupokei fedha  yoyote ile “

Alisema  hakuna usumbufu  wowote  wa kupata hati   hiyo  kwani ndani ya wiki tatu pekee kwa  waombaji wa  mikoani wanaweza  kupata pass  zao baada ya  kukamilisha taratibu  zote  na wale  wanaohitaji hati ya   haraka wanaweza kupewa ndani ya muda  mfupi  zaidi .

 Ng’ondya alisema  mwombaji anayehitaji kupata hati hiyo hatua ya  kwanza anapaswa kuingia katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji www.immigration.go.tz na kisha kwenda katika kitufe cha e-Services.

wakati atua ya pili   mwombaji atapaswa kuchagua fomu ya maombi ya hati tatu, kuchagua ombi jipya, nne, atatakiwa kutiki kiboksi kukubaliana na maelekezo na tano anaanza kujaza taarifa zake kwa ukamilifu ukifuata maelekezo na mpangilio katika kila kipengele.

Baada ya mwombaji kukamilisha kujaza taarifa zake, atafahamishwa ya kwamba usajili umekamilika na kupatiwa namba ya ombi, ambayo ni muhimu aiandike pembeni na kuihifadhi kwa kumbukumbu za baadae.

Kuwa  mwombaji atapewa namba ya kumbukumbu ya malipo na kutakiwa kwenda kulipia malipo ya awali Sh20,000.

Hata  hivyo  alisema  baada ya mwombaji kumaliza hatua hiyo, ukurasa huo, ataingia katika menu ya M-Pesa/Tigopesa (*150*00#/*150*01#).

Amesema baada ya hapo atatakiwa kubonyeza namba 4 (lipa kwa M-Pesa) au kubonyeza namba 4 (kulipia bili)-Tigo na baada ya kuchagua mtandao wa malipo, atatakiwa kuingiza namba ya kampuni 888999 na mwombaji atatakiwa kuingiza kumbukumbu namba (Ingiza Control Number inayoanzia na 99109…….), kisha kiasi (kama ilivyo elekezwa mfano: 20,000), atapata maelezo kuwa unalipa pesa NMB, baada ya hapo ataingiza namba ya siri, atahakiki na kupata ujumbe mfupi wa maneno kutoka M-Pesa/Tigopesa kama muamala umekubalika.

kuwa baada ya hatua hiyo mwombaji atapata ujumbe kutoka kwenye mfumo namba 15200 kama muamala umekubalika, kisha kurudi katika ombi linaloendelea na mwisho ataingiza namba ya ombi au simu na namba ya risiti na hapo atapakua fomu yake ya maombi na baada ya kuwa amepata fomu atatakiwa kuiwasilisha katika ofisi ya Uhamiaji  wilaya ya Mufindi ,Ilula kwa wilaya ya Kilolo ama makao makuu ya mkoa mjini Iringa .