Home Mchanganyiko UGONJWA WA KIWELE WASHAMBAMBULIA MIFUGO NJOMBE

UGONJWA WA KIWELE WASHAMBAMBULIA MIFUGO NJOMBE

0

NJOMBE

Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe wameiomba serikali kupeleka madaktari wa mifugo wa kutosha ili waweze kusaidia kutibu na kudhibiti ugonjwa wa Kiwele ambao umeibuka na kuathiri mifugo mingi katika wilaya nyingi za mkoa huo.

Wafugaji ho wametoa kilio hicho mbele ya katibu mkuu wa wizara ya mifugo na uvuvi prof Elisante Olegabriel alipotembelea na kukagua mradi wa kiwanda cha maziwa mkoani Njombe kilicho chini ya chama cha ushirika cha wafugaji wa Njombe NJORIFA ambapo wameiomba serikali kuona namna ya kuwasaidia kumaliza changamoto hiyo.

Matha mlelwa ambaye ni mfugaji bora 2019 na Walter Mwanyika ambaye ni mwenyekiti wa chama cha wafugaji mkoa wa Njombe NJOLIFA wamesema kuwa kuibuka kwa ugonjwa huo kumeathiri kwa kiasi kikubwa kiwango cha uzalishaji wa maziwa huku pia wakihitaji elimu zaidi ya mifugo.

Mbali na magonjwa kutajwa kuwa kikwazo katika maendeleo ya sekta ya maziwa nae Mark Tsoso ambaye ni mkurugenzi wa mradi wa kuendeleza sekta ya maziwa africa mashariki EADD amesema changamoto nyingine ni masoko ya uhakika huku meneja wa kiwanda cha maziwa Njombe Edwin Kidehele akitaja hatua ambazo zimechukuliwa kukabiliana na hali hizo.

Nae katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi prof Elisante Olegabriel akizungumza mara baada ya kukagua kiwanda hicho na kusikiliza changamoto zinazoikabili sekta ya maziwa mkoani humo ikiwemo magonjwa na masoko anatoa agizo kwa katibu tawala mkoani humo kuwataka maafisa mifugo kutembelea wafugaji na kuwapa elimu ya ufugaji,masoko na matibabu ya mifugo .